Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Mwaka 1979, Simba Sc ya Tanzania ilipangwa kucheza na klabu ya Mufulira Wanderers ya Zambia katika michuano ya CAF.
Mechi ya kwanza katika dimba la taifa ( sasa uhuru ) Simba likufa 4-0
Mashabiki walisononeka sana wakaisusa timu yao. Kikosi kikaendelea na maandalizi ya mchezo wa marudiano.
Simba wakasafiri kuelekea Zambia kimya kimya bila presha wala nini. Siku ya mechi ikawadia huku wakiwa hawana cha kupoteza.
Umma wa mashabiki wa soka nchini Zambia wakajitokeza kwa wingi katika dimba la Independence kushuhudia mchezo huo huku wakiongozwa na Rais wa wakati huo, Kenneth Kaunda almaarufu kama "KK"
Simba chini ya kocha mzawa marehemu Joel Bendera wakafanya come back ya kushangaza.
Mufulira akafa 5-0 mbele ya Rais Kenneth Kaunda. Wachezaji wa Simba waling'aa sana wakiongozwa na George Kulagwa "Best" na Thuwein Ally ambao walikuwa ni sehemu ya wafungaji siku hiyo.
Nimeandika hayo kukumbushia kuwa come back sii jambo rahisi kama baadhi wanavyodhani kuelekea bonanza la jumamosi usiku.