Simba ndiyo Wamefeli Mechi ya Jana

Simba ndiyo Wamefeli Mechi ya Jana

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Baba Jeny bye bye

Wakati stori kubwa ikiwa ni Inonga na Mayele huku wakisahau pia kulikuwa na Chama ambae hakufurukuta mbele ya kibwana, wakati wakisema kuwa hajatetema wanasahau kuwa Morison alikuwa mchezaji wa 12 wa Yanga ( alikuwa msaada zaidi ya Yanga kuliko Simba kwa wale waliofuatilia mchezo kwa jicho la tatu), wakati watu walimsifu Inonga wanajisahaulisha kuwa Mugalu,Bocco na Chama walikuwa na zero impact. Hili ndilo tatizo la kutocheza na hesabu. Alichokuwa anafanya Inonga ni Sawa na mashindano ya kuchagua kikosi cha Timu ya Taifa na sio kuipigania timu kutetea Ubingwa. Anacheza Sana na jukwaa badala ya kucheza na hesabu.

Hii mechi ilikua Ina umuhimu zaidi kwa Simba kuliko Yanga. Niliwashangaa mashabiki pamoja na beki Inonga kuishangilia kwa nguvu zote baada ya dakika 90 huku wakisahau kuwa gap linabaki vile vile. Hii inaiwekea Yanga nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa.

Nilidhani Simba watahuzunika sana kwa Sababu hata kama Yanga wangetwaa Ubingwa lakini wao (Simba) kuwa timu ya Kwanza kuifunga Yanga msimu huu lingekuwa jambo la amani Sana miongoni mwa mioyo ya mamilioni ya wanasimba.

Kiufupi Ubingwa usingenoga. Kwa mantiki hiyo Simba Jana walifeli na Yanga walifaulu.
 
Yaani unawaza mambo ambayo simba walishaachana nayo siku nyingi sanaa, eti kuwa wa kwanza kuifunga yanga
 
Na msimu huu yanga akiwa bingwa anavuna mpunga wa maana, zawadi ya ubingwa Mil.500, bonus kwenye mkataba wa Azam Mil.500, apo tiyali bil.1 bado wadhamini wengine awajaweka mpunga wao kama sportpesa,Gsm, ivyo msimu huu yanga ina bahati kubwa kutwaa ubingwa na kulamba mabilioni ya pesa
 
Na Simba atavuna ngapi kwa kuwa mshindi wa pili na robo fainal shirikisho plus bonus
 
Na Simba atavuna ngapi kwa kuwa mshindi wa pili na robo fainal shirikisho plus bonus
Mara paap Simba inefungwa na Namungo, Kagerra, Geita, mbeya city na Azam
 
Yaani unawaza mambo ambayo simba walishaachana nayo siku nyingi sanaa, eti kuwa wa kwanza kuifunga yanga
FB_IMG_16514643879728793.jpg
 
Na msimu huu yanga akiwa bingwa anavuna mpunga wa maana, zawadi ya ubingwa Mil.500, bonus kwenye mkataba wa Azam Mil.500, apo tiyali bil.1 bado wadhamini wengine awajaweka mpunga wao kama sportpesa,Gsm, ivyo msimu huu yanga ina bahati kubwa kutwaa ubingwa na kulamba mabilioni ya pesa
Kama simba walivyojisifia kwenye VAR, hata sisi tuna kila sababu ya kukisifia kama timu ya kwanza kuvuna mamilioni ya shilingi kutoka kwa mmoja wa wadhamini wa Ligi kuu.
 
Back
Top Bottom