Simba nendeni Misri kukamilisha ratiba. Ukuta wa Yericko umegeuka kuwa ukuta wa biskuti, kila mechi bao

Simba nendeni Misri kukamilisha ratiba. Ukuta wa Yericko umegeuka kuwa ukuta wa biskuti, kila mechi bao

Mechi bado haijaisha, Simba kutandikwa tano pale Cairo halitakua jambo jipya.
Mbaya zaidi mwekezaji wenu mlipo pata goli akawa anajipiga kifuani mbele ya Rais wa Ahly, yaani alikua ana mtambia.
Sasa kile kitengo kinaweza kikasababisha mtandikwe ata zaidi ya tano pale Cairo.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Zisipofika hizo 5
 
Uliyaona hayo matunguri? Imani potofu zimejaa kwenye mafuvu yenu, kipi cha ajabu? Yaani wao kukosa goli wamelogwa?

Ujinga mtupu, football imechezwa vizuri kwa ufundi.
Kwa hiyo na ihefu uchwai wao wametoka wapi!? Rais mwenyewe wa FIFA katumia muda kujifunza kauli mbiu ya Nguvu moja...Tumepishana mbele ya uongozi wote Africa na dunia Simba ni timu kubwa duniani...na tukienda kule ni kamoja Ka haja...
 
Nilikuwa nawashangaa sana mashabiki wa hii timu walivyokuwa wanatamba sana mitaani wakijiapiza kumfunga Aly ahly goli za kutosha!

Lakini kwa wale wanaojitambua tulikuwa tunajua madhaifu ya mwakarobo na lilikuwa ni suala la muda tu kuzima tarumbeta zilizokuwa zinapigwa na vijana wa Rage, Baada ya dk 90 wimbo umebadilika umekuwa ule ule wa miaka yote waliyozoea kuuimba wa "TUMEKUFA KIUME"

Tokea nizaliwe sijawai kuliona ilo kombe la Kufa KIUME. Leo Mwakarobo Mganga wao alichowasaidia ni kupunguza idadi ya MAGOLI, kitendo Cha Aly Ahly kukosa zile nafasi 3 za wazi kwa macho ya kawaida unaweza ukadhani ni bahati mbaya lakini Ile ilikuwa ni kazi ya sangoma!

Ahly Ahly ilikuwa wambutue mtu goli 5 Leo but Mganga kaepusha aibu kubwa Leo. Na zile zilizokoswa wangekuwa kwao MISRI zilikuwa ni kamba kwa kuwa siku zote uchawi aupandi ndege ndio maana tulikuwa tunashuhudia sana zile goli tano tano kipindi kile!

Ndani ya mechi 8 ukuta wa yeriko umeruhusu kamba 9 kuchana nyavu zake, ndio maana tunasema safu Bora ya ulinzi itakupa makombe na safu Bora ya ushambuliaji itakupa magoli tu!

Mwakarobo najua mtakuja na mapovu kama yote lakini ayanibabaishi nawapa vidonge vyenu mkipenda mvimeze mkipenda mvitapike, timu yenu Ina shida kubwa kwenye eneo la kiungo mkabaji, uyo Ngoma mliyeenda sijui kumuiba uwanja wa ndege kwa mujibu wa msemaji wenu anaweza kutamba kwenye mechi za wakina JKT Tanzania na sio mechi kubwa za kimataifa, mechi za kimataifa utamuona Kama timu inamiliki mpira lakini Kama timu inapekekewa moto ni sawa na yale mapazia ya buku buku yanoyouzwa mnadani!

Sasa keshokutwa mnakwenda Misri kukamilisha ratiba yenu kwakuwa kule akuna kuvunja Nazi Wala kuchoma uwanja uwezo wenu halisi unakwenda kuonekana mjipange na Ligi kuu na makundi ya klabu bingwa!

MAPOVU YA OMO NA KLEESOFT YANARUHUSIWA KWA WAFUASI WA MBUMBUMBU!
Masikini nyumamwiko mumeshasahau kuwa na nyie wanawasubiria kwenye makundi. Bora ukose mali lakini upate akili
JamiiForums1020740303.jpg
 
Hizo ngonjera peleka kwa akina mama wenzio huko, huku hatuhitaji wanawake kwenye shughuli za kiume pitisheni bakuli kama ilivyo kawaida yenu tuwachangie mkalipie deni la upumbavu wenu, shwuaini
 
Masikini nyumamwiko mumeshasahau kuwa na nyie wanawasubiria kwenye makundi. Bora ukose mali lakini upate akili View attachment 2787633
Usiwe unafananisha kichuguu na mlima Babu, Kaa kwa kutulia usubilie iyo timu iliyokutoa kamasi itapokutana na wanaume yanga, najua ili kenge ajue amejuruiwa ni mpaka aone damu, mtafurahishwa siku sio nyingi!
 
Kama BODI ya SIMBA itaendelea kumvumilia huyu ROBERTNO, ..itakuwa ndiyo hivyo kabisa..

Tusubiri aibu ndipo mkurupuke....
 
Hao waarabu unaowasifia ndio hao hao tuliowaona au kulikuwepo na mechi nyingine unaangalia kwako?
 
Usiwe unafananisha kichuguu na mlima Babu, Kaa kwa kutulia usubilie iyo timu iliyokutoa kamasi itapokutana na wanaume yanga, najua ili kenge ajue amejuruiwa ni mpaka aone damu, mtafurahishwa siku sio nyingi!
Wewe kakune nazi tu umpikie mumeo ugali
 
Back
Top Bottom