Simba ni chachu ya mafanikio ya Yanga, nashauri serikali ifanye hivi

Simba ni chachu ya mafanikio ya Yanga, nashauri serikali ifanye hivi

PakiJinja

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
11,689
Reaction score
25,848
Iingeze idadi ya watu itakao wasafirisha kwenda kushangilia first leg ya fainali, na safari hii iongeze 55 wengine watakaopenda kwenda kuishangilia timu itakayopambana na Yanga.

Maamuzi ya mashabiki wa Simba yamekuwa ni chachu sana ya ushindi kwa Yanga, ndiyo maana nasisitiza wale wote wasiopenda mafanikio ya Yanga maadam ni watanzania, nasi na wao wasafirishwe.

Naliongea hilo sababu mabadiliko makubwa ndani ya Yanga yalizingatia pia kwa karibu mafanikio waliyoyapata wenzao wa Simba.
Ni ukweli usiofichika kuwa Simba walifikia hatua nzuri sana kisoka, waliondokana na lile soka la kijadi ambalo lilitegemea Mwenyekiti na mbinu zake za kiasili, safari hii Simba walikua more strategic, wakichora taswira ya soka la kisasa, ni bahati mbaya kwamba kuna ile 'Indian Janja Janja' kwa mbaali, ila inahitaji busara sana kukipita kipindi hiki.
Inawahitaji Simba kutoumizwa na mafanikio ya Yanga ili waimarike zaidi, lakini wakiruhusu kuumizwa na mafanikio ya Yanga najua kitakachofiata na bakora pale klabuni ni wadhamini kuwaachia timu. Hili sipendi litokee, maana kimataifa sasa hivi Simba inazungumzika, ni kati ya vigogo wa soka barani Afrika, itakuwa ni fedheha sana wakianguka kutoka pale walipo.

Alamsiki!
 
Nipeni mau yangu kwaza mimi yanga napita kuchukua maua yangu ndio nitachangia mada af wanasimba wote pisheni njia wanaume tunapita hapa
 
Chachu? Are you normal?
2103327492.jpg
 
Back
Top Bottom