Tusijipe moyo sana tukabweteka huku tukiamini tumevuka next round,matokeo yake tutakua tunaishia hapahapa robo fainali,Msimu uliopita comments zilizokua ktk page ya kaizer chiefs za wao wenyewe wasouth zilikua hivihivi tena mashabiki wao walifanya maandamano hadi klabuni wakishinikiza uongozi uachie ngazi,na kocha wao afukuzwe japo walifika robo,sisi kuona vile tukabweteka matokeo yake tuliyaona.Timu za south hata zikiwa vibaya still ubora wao wa ligi unawabeba,angalia timu ya amazulu msimu huu japo haijavuka next round ila walikua wazuri sana.Muhimu tusidharau timu yoyote itakayokuja awe ahly Tripoli,au mazembe ambaye hatujawahi wafunga.