Simba pale kwa Che Malone tumepigwa

Simba pale kwa Che Malone tumepigwa

Labda mechi zitakazofuata..
Lakini mechi hizi za SIMBA , bado uwezo wa kutengeneza nafasi ni mdogo.
Nawaza SIMBA ya PABLO ile ya akina Larry Bwalya, CHAMA, Micquson, walivyokuwa wakitengeneza vyumba ...Shida ikawa tu finishing za Mugalu.

Leo simba wapo finishers wazuri, PHIRI ,BALEKE...lakini clear chances unaitafuta kwa tochi..
 
Haya YOTE niliisha yasema kiufundi.

1. NILISEMA Simba walitakiwa kumbakisha Kakolanya, au watafute Golikipa wa kigeni.

2. Simba hakuna Beki wa kushoto, wakashindwa Hadi kwa YAHAYA Mbegu.

3. Simba Hakuna Beki wa kumchallange Inonga au Malone endapo wakishuka kiwango, WAKIUMIA au wakiwa na ADHABU.

4.TATIZO KUBWA LA SIMBA NI HAPA KATIKATI KWENYE KIUNGO MKABAJI NO 6. CDM.
NGOMA ANGEKUWA NA BANGALA SIMBA INGECHEZA FAINALI.
Kwa mechi mbili nlizotazama za Simba.

1. Ni kweli kabisa namba 3 haipo, jana mpira umechezwa sana kwenye zone ya Zimbwe, na amekuwa ni njia.

2. Ally Salum hakuna kipa pale, ni vile ndani ya mechi mbili hizi hakupata ushindani ila angekutana na safu nzuri au kashkash alokutana nayo jana Beno, Simba angekaa hata 3.

3. Namba 6 ya Simba, eneo la ukabaji mbali na Mzamiru ambaye umri umeenda na anatumia nguvu nyingi, Kanoute ana kazi ya ziada. Simba inahitaji mtu hasa wa kutuliza lile eneo la ukabaji.

4. Yule Fabrice Ngoma ni mzuri sana, hasa timu ikiwa inashambulia au inapossess. Mbali na hapo ni mzigo sababu hakupi attribute kubwa kwenye ukabaji.

5. Simba ina wings wengi lakini sehemu kubwa zaidi tunaona Saido ndo mwenye mchango, siku Saido akawa nje na Chama, timu inaweza ikawa kwenye wakati mgumu ktk utengenezaji wa nafasi.

6. Taratibu nimeanza kukuelewa ulivyokuwa unaponda usajili wa Simba.

7. Tukutane J2 mtani.
 
Simba wamejaza Mawinga bila kuwa na kiungo mkabaji

Makosa Lazima yatokee kwa Mabeki.
Hakuna kiungo WA MAANA WA kuweza kuilinda ukuta ( Back 4)

Viungo wote WA Simba ni BOX TO BOX.
wanaacha nafasi Yao wanapanda juu na kuacha Mabeki wakiwa One against One na Mabeki.

Katikati panapitika mno.
Kanute na mzaminu ni njia
Kwa ile Simba ya jana, wangekutana na Azam pasingetosha. Jana mid za Simba zilipotea hasa mipira wakipoteza.
 
Saido alifikisha magoli 4 kimataifa tofauti magoli 3 na Mayele.

Mayele hakuwa mfungaji Wa maajabu kama mnavyotaka ionekane.

Hata Magoli ya wafungaji Bora Ligi Kuu kama John Bocco au Meddie Kagere hakuweza kuyafikia
Magoli yapi alifunga Saido kwenye mechi za CAF achana na hayo ma nne nitajie moja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Itoshe wewe kuitwa mpuuzi.
Kwa Mantiki ipi nastahili kuitwa mpuuzi na nimepuuzia nini?

Mayele alikuwa Wa kawaida sana na ndiyo maana kashindwa kuzifikia rekodi za kina Kagere na Bocco walipokuwa kwenye viwango vyao vya Juu.
 
Kwa Mantiki ipi nastahili kuitwa mpuuzi na nimepuuzia nini?

Mayele alikuwa Wa kawaida sana na ndiyo maana kashindwa kuzifikia rekodi za kina Kagere na Bocco walipokuwa kwenye viwango vyao vya Juu.
Ameweka record ya kuuzwa bei kubwa kuliko mchezaji yoyote kwenye ligi ya bongo, usisahau kunitajia goli moja tu alilofunga babu Saido kwenye mechi za CAF ukikosa nitajie hata assist moja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom