Simba pale kwa Che Malone tumepigwa

Simba pale kwa Che Malone tumepigwa

Yaani ni mechi mbili tu zimechezwa, lakini kama mtu una jicho la ufundi wa kimpira utagundua hili mapema sana.

Mechi dhidi ya power dynamos, Che Malone alifanya makosa mawili ya wazima ila wale washambuliaji wa power dynamos wakapoteza nafasi. Jana pia kafanya makosa mawili ya wazi kabisa.

Sasa hapa Simba inatapambana na Timu za daraja la kawaida kabisa, huko Super Ligue na Champion league sijui itakuaje. Kiufupi huyu jamaa sio mmbaya sana lakini naona kwa level za Simba Bado sana.

Hawa watangazaji wanatoa sifa za kijinga tu eti electrical fence, kumbe ukuta wa makuti tu.
Hakuna binadamu aliyekamilika acha ufala weye. Yaani mechi mbili ushahitimisha kuwa tumepigwa yaani akili huna kwelikweli.
 
Namaanisha anakuzwa sana. Misimu yote miwili hakuwa mfungaji Bora peke yake na Wala wastani wake Wa kufunga Kwa mechi haukuwa mkubwa sana.

Ila umaarufu wake uliletwa na kutetema anapofunga!!
Hili la kuwa sio mfungaji mzuri sana ni sawa, ila kuhusu ushambuliaji bora, kwa maana ya kuitendea haki nafasi ya straiker na maarifa kama mchezaji alikuwa kwenye daraja la juu sana!
 
Hili la kuwa sio mfungaji mzuri sana ni sawa, ila kuhusu ushambuliaji bora, kwa maana ya kuitendea haki nafasi ya straiker na maarifa kama mchezaji alikuwa kwenye daraja la juu sana!
Yap!! Kwenye hoja ya kwamba alikuwa ni " aggressive Striker" hilo halina mjadala.

Kwenye levo ya mshambuliaji mpambanaji Mayele ana silka kama ya kina Kagere, Ronaldo ama Haaland.
 
Mbona una lazimisha hoja yako ndio watu wa amini .?
Yani una tukana watu kubwa ni wajinga na wapumbavu kisa kukataa mawazo yako?
Simba hii msimu uliopita ikiwa na Mzamiru na Kanoute walifungwa goli chache kuliko timu yoyote ligi kuu na pia hata ligi ya mabingwa Afrika waliondolewa kwenye matuta.
Kifupi Simba ni nzuri sana, hizi mechi za Mwanzo tegemea kuona timu ilicheza kawaida kwa sababu nyingi kwanza wageni wana ingia kwenye mfumo taratibu taratibu.
 
Ukiwa hauna uelewa wa mpira wa miguu una toa maoni kila jambo.
Simba imecheza High Pressing kwa maana timu yote ina sogea juu mpaka kwenye msitari ya katikati ya uwanja na kuacha eneo kubwa kati yake na kipa.
Timu inayo cheza hivi mabeki wa pembeni wana tumika zaidi kushambulia sio kukaba.
Nenda kaangalie Liverpool inavyo cheza, namba Sita na na mabeki wa kati ndio wanaziba mashimo ya mabeki wa pembeni.

Simba ndio kwanza wamecheza mechi ya kwanza ya mashindano rasmi msimu huu lakini maoni ni kama wameisha cheza mechi 10 za msimu.
Kocha yoyote mzuri wachezaji wapya wana ingia kwenye mfumo taratibu taratibu sio kuingiza wachezaji wapya wengi kwenye kikosi.
Mchezaji kama Kramo hajacheza kabisa, Luis miqisoun ndio kwanza ana pewa dakika chache kwanza ili aingie kwenye mfumo.

Kuhusu Ally Salimu kwamba sio kipa anaefaa kuwa Simba ni kumkosea adabu, Kucheza mechi na Yanga msimu uliopita Yanga ikiwa na Mayele na Nyota wake wote, na Yanga ikafungwa.
Kacheza ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Taifa Simba ikashinda ugenini kafungwa moja tena mechi nzito kweli ilikuwa.
Ulitaka mikimiki ipi labda akutane nayo ili ndio useme yeye ni kipa mzuri ?

Mechi za Mwanzo wa msimu zisikuchangaye ukaona timu fulani ni nzuri au mbovu.
Maana wapo wachezaji wana Chelewa kuchanganya na wapo wanao wahi kuchanganya.
 
Kama wewe unavyo hitaji maombi maana una mtindo wa ubongo unao julikana kama Amfifilo.
 
Back
Top Bottom