Simba robo fainali CAF kukutana na CR Belouizdad, Kaizer Chiefs au MC Alger

Simba robo fainali CAF kukutana na CR Belouizdad, Kaizer Chiefs au MC Alger

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Sasa ni rasmi mpinzani wa Simba katika robo fainali ya CAF Champions League ni lazima awe mmoja kati ya timu hizi tatu; CR Belouizdad ya Algeria, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini au MC Alger ya Algeria pia.

Hii ni baada ya mechi za makundi yote manne kumalizika leo na timu hizo kushika nafasi za pili sambamba na Al Ahly ya Misri ambayo hata hivyo haiwezi kukutanishwa na Simba kwa kuwa zinatoka katika kudi moja. Droo ya kumpata mpinzani mahususi itafanyika tarehe 30/04/2021. Misimamo ipo hivi:

1618093568110.png
 
Points 13 alizo nazo Simba dhidi ya wapinzani wake wenye points 9 zitambeba sana
 
Hizo timu zote zilizofuzu.. bingwa anaenda kuwa esperence... kama unabisha tunza hii comment
Hamjaanza hizi ramli leo, tangu enzi za Plateau ya Nigeria tulizisikia na wengine wakaahidi kutembea uchi. Hapa tunazungumzia kuingia nusu fainali, wewe unazungumzia ubingwa! Upo nje ya mada kabisa. Esperance watamalizana mapema tu na Ahly robo fainali, Simba amewafanyia kitu kibaya sana maana amewalazimisha wababe wakutane mapema kwa kumuacha Ahly nafasi ya pili
 
Hamjaanza hizi ramli leo, tangu enzi za Plateau ya Nigeria tulizisikia na wengine wakaahidi kutembea uchi. Hapa tunazungumzia kuingia nusu fainali, wewe unazungumzia ubingwa! Upo nje ya mada kabisa. Esperance watamalizana mapema tu na Ahly robo fainali, Simba amewafanyia kitu kibaya sana maana amewalazimisha wababe wakutane mapema kwa kumuacha Ahly nafasi ya pili

Hongereni simba.. ndani ya misimu mitatu inayofatana mmefika robo fainali mara mbili... esperence ndani ya misimu mitatu hiyo hiyo mliyofika robo ametwaa ubingwa mara 2.. na timu ni ile ile haijabadilika.. why kwenye prediction mtu akiwapa nafasi ya kuwa mabingwa tena wewe unakasirika... kwenye comment ile sijaiponda timu yeyote.. nimeweka prediction yangu. Ila wewe unakasirika huku kuna timu 7 sijazipa nafasi ya ubingwa.. why wewe mmoja ujistukie
 
Hongereni simb.. ndani ya misimu mitatu inayofatana mmefika robo fainali mara mbili... esperence ndani ya misimu mitatu hiyo hiyo mliyofika robo ametwaa ubingwa mara 2.. na timu ni ile ile haijabadilika.. why kwenye prediction mtu akiwapa nafasi ya kuwa mabingwa tena wewe unakasirika... kwenye comment ile sijaiponda timu yeyote.. nimeweka prediction yangu. Ila wewe unakasirika huku kuna timu 7 sijazipa nafasi ya ubingwa.. why wewe mmoja ujistukie
Umeongea vizuri mkuu na kila mtu anapaswa kuheshimu mawazo ya mwingine Ila sidhani kama uko sahihi kusema kama unabisha save hii comment, kubashiri inabaki kuwa kazi ngumu kuliko zote hasa kwenye mpira, me naweza kusema pia esperence anaweza kuwa bingwa Ila sio Kwa kukazia namna hiyo maana ata mie ningesema kuwa "Simba anaenda kuongoza kundi lake kama unabisha save hii comment" we ungejibu vp hii comment?
 
Kwa upande wangu ningetamani Simba apewe kaizer chiefs, hawa jamaa uwezo wao ni kawaida compared na team zingine zilizovuka stage ya makundi, Kwanza hawana uzoefu kulinganisha na team zingine lakini pia hawana wachezaji hatari kama team zingine, japokuwa walipata ushindi dhidi ya Waydad ila hiyo haiondoi maana ya kwamba wao ndo kila mtu anawatamani

Hatua inayofata hao jamaa wa ngozi nyeupe (warabu) ukitoa mamelodi, warabu ni hatari Sana, wanaijua vizuri sana hii michuano lakini pia Wana mbinu nyingi Sana za kushinda hizi mechi kubwa, Ila Kwa kaizer chief yule Simba anammudu vizuri tu, kuanzia Hali za hewa kwao na bongo, mida ya game za kwao na kwetu almost the same, Simba at least anatakiwa kukutana na mwarabu nusu fainali ila akikutana nae robo kibarua kinaenda kuwa kigumu
 
Back
Top Bottom