Simba S.C yashusha kipigo kizito tena Leo.. Wapinzani kaeni Chonjo.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Huu moto aliouwasha Kocha Bora kabisa toka Kameruni, Joseph Omog, akisaidiwa Kocha bora kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini Uganda, Jackson Mayanja sijui ni nani mwenye uwezo wa kuuzima. Simba S.C imeimarika sana kwa sasa.

Baada ya kugawa dozi nzito nzito kwa Polisi Moro, Moro Kids.. leo ilikua ni zamu ya timu bora kabisa kwa sasa Mkoani Morogoro, Bukinafaso kupewa stahiki yao.. na hii ni baada ya kutandikwa goli 5-0 bila hata chembe ya huruma.

Wafungaji wa magoli katika mechi ya Leo ni Mousa Ndusha, Shiza Kichuya, Said Ndemla na Ibrahimu Ajibu katupia goli 2 kambani [nasisitiza huyu jamaa ule ugonjwa wake kufunga unaendelea kua sugu kila siku zinavyosonga].

Mpaka sasa.. Simba chini ya Omog.
1. Mechi Tulizocheza - 3
2. Magoli Tuliyofunga - 15
3. Magoli Tuliyofungwa - 0
4. Aina ya Soka - Soka la Kasi, Pasi Nyingi, Ufundi Mwingi n.k

... and the cycle continues.
 
Hongereni mikia kwa ushindi dhidi ya Burkinafaso ya Matombo Morogoro
Shukrani Mkuu.. Moto tushauwasha, sijui ni nani atakayethubutu kuuzima.
duuh...kwa aina hii ya mashabiki lazima aveva na hanspopu wafurahi
Ushindi huu, lazma upokelewe kwa furaha na wanazi wote wa Mnyama popote walipo katika dunia hii.. Ila kwa upande wa jagwani, ushindi huu unawafanya waanze "kupoteana".
 
Maujiko mengine haya, timu yenyewe ni toka matombo.
Kwa sasa huwezi elewa huu ushindi una maana gani.. Karibu Taifa Stadium, 08.08.2016 ushuhudie jinsi tunavyoiadhibu kisawasawa timu bora kabisa kwa sasa toka nchini Angola.
 
Dah Mkuu inaelekea wakina Aveva na Hans Pope wamekupa hii kazi maalumu kwenye mitandao kila kabla ya msimu wa ligi kuanza. Maana nakumbuka hata msimu uliopita ulikuwa unatuletea habari hizi hizi za kuwapumbaza wana Simba cha kushangaza ligi ilipokaribia kuisha na maji kuzidi unga ulikimbia kabisa hapa Jukwaani mpaka tukawa tunakutafuta kwa tochi. Lakini hongera hii kazi ya ukasuku unaiweza sana Sembo.
 
Kwa sasa huwezi elewa huu ushindi una maana gani.. Karibu Taifa Stadium, 08.08.2016 ushuhudie jinsi tunavyoiadhibu kisawasawa timu bora kabisa kwa sasa toka nchini Angola.

Timu gani kutoka Angola,FC Liboro?
 
Nakupata mkuu, najua tumenyanyasika kwa muda mrefu na hio imetokana na ubinafsi wa vongozi wetu, ila kwa matombo sio level yetu kiasi kwamba tuanze kujipa matumaini mapema kihivyo.
Simba ni simba tu hata akiwa mzee anabaki kuwa simba.
 
Shukrani Mkuu.. Moto tushauwasha, sijui ni nani atakayethubutu kuuzima.

Ushindi huu, lazma upokelewe kwa furaha na wanazi wote wa Mnyama popote walipo katika dunia hii.. Ila kwa upande wa jagwani, ushindi huu unawafanya waanze "kupoteana".

Angali usije kupotea wewe tuu kama ilivyokuwa msimu ulioisha,maana ulikimbia kabisa hapa Jukwaani.
 
Nakupata mkuu, najua tumenyanyasika kwa muda mrefu na hio imetokana na ubinafsi wa vongozi wetu, ila kwa matombo sio level yetu kiasi kwamba tuanze kujipa matumaini mapema kihivyo.
Simba ni simba tu hata akiwa mzee anabaki kuwa simba.

Mwenzako Sembo ameshalitambua kuwa level yenu nyie kwa sasa ni hizo timu za Matombo,sio Yanga wala Azam tena ndio maana kila siku anatuletea habari za ushindi wenu wa mchangani hapa.
 
Timu gani kutoka Angola,FC Liboro?
Si Liboro Mkuu.. Tutapambana na kiboko ya Liboro, wanaitwa Grupo Desportivo Interclube a.k.a Interclube
Angali usije kupotea wewe tuu kama ilivyokuwa msimu ulioisha,maana ulikimbia kabisa hapa Jukwaani.
Mkuu Msimu uliopota sikukimbia, ila majukumu tu yalizidi.. Msimu huu tutakua pamoja.
 
Mwenzako Sembo ameshalitambua kuwa level yenu nyie kwa sasa ni hizo timu za Matombo,sio Yanga wala Azam tena ndio maana kila siku anatuletea habari za ushindi wenu wa mchangani hapa.
Ni jukumu langu kuwafahamisha Mashabiki wa Simba S.C popote walipo katika sayari hii, juu ya maendeleo ya timu yao.. Hivyo hata hizi Mechi za kirafiki tunazocheza, ni haki yao kupata matokeo.
 
Ni shiiida sana, unapojisifia kuongoza kwa ubora kwenye darasa la wajinga! Utakuwa na fikra kama hizi!
Unatakiwa ufahamu hii ni Pre-Season.. Kama inshu ni Mnyama kuongoza katika darasa la wajinga.. Karibu Taifa Stadium, siku ya Simba Day.. Tutakapokua tunatoa onyo kali kwa wapinzani wetu. Nadhani siku hiyo, Tanzania itajua, na Dunia itajua kua Simba S.C ya sasa ni weka mbali na watoto.
 
Hahaha Mkuu unachekesha sana aisee,sasa kwanini usipewe nafasi ya Uafisa Habari wa Wamatopeni?
 
Back
Top Bottom