Simba sasa hivi inacheza mpira makande

Simba sasa hivi inacheza mpira makande

Nawasalimia wana Msimbazi wenzangu!

Nimesikitishwa na mpira unaochezwa na timu yetu pendwa ya Simba (Lunyasi), timu siku hizi inacheza mpira mbaya sana, mpira makande, magoli yetu yenyewe yanapatikana kipapatupapatu kama ya utopolo. Leo nimeona takwimu eti Simba katika mechi 2 za ligi ndo tunaongoza kwa kupiga cross (cross 34!) Tangu lini Simba ikaongoza kwa kupiga cross na sio kupiga pass?

Kuna watu watakuja na utetezi kuwa timu Ina wachezaji wapya wengi, hivyo hawajaingia kwenye mfumo wetu wa Lunyasi. Hii sio kweli, maana ukiangalia kwenye timu iliyoanza (first eleven) ni wachezaji wawili tu ndo wageni ambao ni Inonga na Kanoute, lakin wengine wote ni walewale wapo zaidi ya misimu miwili. Na hata wanaosema kuondoka kwa Luis na Chama ni sababu ya timu kucheza hovyo siku hizi, nayo sio kweli, kuondoka kwa wachezaji wawili hakuwazuii watu kupiga pass na kucheza mpira uliozoeleka, maana hata hao wachezaji wawili walikuja waliikuta timu inacheza mpira biriani.

Tatizo kubwa ninaloliona ni kocha. Gomez ni kocha anaejali zaidi matokeo (results oriented) kuliko kujali namna ya hayo matokeo yanapatikanaje. Wana msimbazi tumezoea mpira biriani, Gomez alikuja akaikuta timu imetengenezwa na Uchebe na Kishingoo, na yeye akatembelea humo. Na zaidi ni Uchebe ndo aliitengeneza timu iliyocheza mpira biriani tunavyotaka.

Ombi langu kwa uongozi wanatakiwa wamuambie kocha sisi tunataka timu icheze mpira unaoeleweka, na sio mradi kupata ushindi wa style ya utopolo. Magoli ya kona na cross, yanatokana na piga nikupige. Kama Gomez hawezi kutupa mpira tunaotaka atimuliwe!
Mchezo unaoeleweka ni kushinda
 
Tunataka vyote. Mbona zamani tulikuwa tunacheza na tunapata matokeo? Tunataka vyote. Msimu wa 2017/2018 tulichukua ubingwa baada ya kuletwa yule kocha aliyetupa ubingwa kwa kandarasi ya miezi 6 Pierre Lechantre, lakin hakuongezwa mkataba kwasababu alikuwa anatupa matokeo lakin mpira mbovu. Ndo akaja Uchebe akatengeneza hii timu, ikawa inacheza mpira mzuri na ubingwa tunachukua. Sasa huyu Gomez anaturudisha kwenye mpira makande. Hatukubali
Hujitambui wewe. Anzisha timu yako ukapike hilo biriani.
 
Hatua za mtoano zina presha zake, ni tofauti na hatua ya ligi ndefu au makundi ambapo unakuwa na muda wa kujaribu hivi na vile kwa kusahihisha makosa na kuendelea na mazuri. Katika mtoano, ukikosea tu ukakosa goli ugenini au ukaruhusu goli nyumbani, kuna hatari hata ya kukosa fursa ya kuja kuonyesha biriani lako kwenye makundi. Mfano mwepesi ni jinsi tulivyoshindwa kupata goli la ugenini katika mechi za mtoano za UD Songo na ile ya Kaizer Chiefs. Mechi hizo mbili kwa miaka miwili tofauti, kama tungepata goli moja ugenini basi tungesonga hatua inayofuata
Tupo hapa..hata kwenye ligi ya nyumbani hii timu itendelea kucheza mpira huohuo. Hata tukiingia makundi hii timu imekuwa mbovu
 
Utopolo ni wewe badala ya kufurahia ushindi unaleta analysis za kijinga. Ulitaka Simba imiliki mpira kama ilivyocheza na Kaizer Chiefs halafu ifungwe magoli manne ili mpate cha kuongea. Hamna akili nyie Utopolo.
Kwahiyo kubutuabutua ndo njia ya ushindi? Mbona As Vita tulimfunga kwao na tulicheza vizuri. Hujui mpira wewe
 
Sasa Lechantre alikuwa na mpira gani ule? Unaweza kumfananisha na Uchebe?
Lechantre....msaidizi wake Akiwa masoud Djuma
3-5-2....ndio mfumo alioutumia. Unasema simba ilikuwa inacheza mpira mbovu...unakumbukumbu vizuri kweli mkuu?
Simba iliyotoka 2-2 na al masry taifa ikatoka
O-0 egypt ( sina hakika hapa) unaiita mbovu?
Unadhani kwanini masoud djuma ni kipenzi cha wanasimba mpaka leo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makolo siku hizi kupiga hata pasi tatu ni mtihani
 
Back
Top Bottom