Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Naaam wasalam,

Ile siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika..leo mtoto hatumwi dukani.

Karibuni katika matukio mubashara(live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa Soka la bongo, Simba na Yanga utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.

Huu ni mchezo wa ligi kuu ya NBC Simba akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Yanga.. mchezo uliopita sa ngao ya jamii Simba aliangukia pua kwa goli moja kwa sifuri kutoka kwa Yanga.

Pia Simba mechi ya mwisho kimashindano imetoka kupoteza 2_1 kutoka Red Arrows na hivyo kufuzu kwa aggregate ya 4-2 katika kombe la Shirikisho Afrika... Yanga ilicheza mechi ya mwisho ligi kuu na Mbeya Kwanza na kushinda 2_0.


Nani ataibuka kidedea, kaa nami hapa mwanzo kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa.

_____________________________________________________________
Updates zaidi kukujia kadiri zinavyopatikana.

>>Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni Hery Sassi na wasaidizi wake kama ilivyotangazwa awali

>>Azam Tv kupitia chaneli ya Azam sports 1 HD watakuwa mubashara (live).

-----------‐-------------------------------------------------
Kikosi cha Simba kinachoanza (STARTING XI)
1. Manula Aishi
2.Kapombe Shomary,
3. Hussein Mohamed ( Captain)
4. Onyango Joash
5. Inonga Henock
6.Mkude Jonas
7. Denis Kibu,
8. Kanoute Sadio,
9. Kagere Meddie,
10.Morrison Benard
11. Dilunga Hassan

Substitute(Akiba): B. Kakolanya, Israel P, Kennedy J, Erasto N, Mzamiru Y, P. Banda, Bocco J, R. Bwalya, Mhilu Y.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo (STARTING XI)
1.Djidgui Diarra
2.Djuma Shabani
3.Kibwana Shomary
4.Mwamnyeto Bakary (Nahodha)
5.Job Dickson
6.Bangala Yannick
7. Aucho Khalid
8.Moloko Jesus
9. Ntibazonkiza Saido
10. Feisal Salum
11. Mayele Fiston

Akiba /Substitute Johora Erick, Bryson David, Shaibu Abdalla, Yassin Mustafa, Mauya Zawadi, Makambo Heritier, Kaseke Deus , Yusuf Athuman, Farid Musa

------------------------------------------------------------------

Karibuni, muda mchache ujao kipute kinaanza hapa Dimba la Mkapa lililofurika mashabiki huku kukiwa na Magepu machache katika baadhi ya viti/majukwaa hapa

>> Timu ndio zinaingia uwanjani hapa kujipanga tayari kuanza soka

01' Mpira umeanza hapa kwa Kasi Yanga wakianza kusukuma gozi la ngombe kuelekea Simba

03' Fiston Mayele anakokota mpira kuelekea Simba ila anadhibitiwa anaanguka kwenye 18 ya simba

06' Yanga wanashambulia lango la Simba, Aishi Manula anachomoa mkwaju pale kutoka kwa Moloko..namna gani pale

08' Morison anacobtol mpira kifuani pale anapiga shuti inakuwa off target

11' Zimbwe anatoa mpira inakuwa kona ya kwanza kwa YANGA inapigwa na Saido Ntibazonkiza.. inapigwa pale inaookolewa na Kanoute..

12' anakokota Morison hadi nje ya box anaangushwa na Job D..

13' Faulu kwa Yanga Simba wanapiga kypitia Morison ila inaokolewa na ukuta mzuri wa yanga

14' Yanick anaangushwa na H Dilunga... Kasi ya mchezo ni kubwa huku wachezaji wakicheza kwa tahadhari

19' Morison anapiga shuti kuuubwa linaenda nje 0ale

22' Feisal anaangushwa inakuwa ni Faulu, inapigwa na Saidoo inaokolewa

24' Faulu kwa Yanga, Onyango njano kadi anapewa kwa kumzuia Mayele.. inapigwa pale aaaaa Aucho anapiga kichwa mpira unatoka nje

27' Yanga wanashtukiza hapa golini, Mayele anakosa control na mpira na kukosa goli hapa..aisee

31' Kapombe S. Yupo chini baada ya kukabana na Saidoo..wakati huo mpira uko nje.. Kapombe anapatiwa matibabu

34' Freekick kwa Yanga, Feisal a naangushwa wnaanza inaokolewa..mpira bado ni wa kasi

40' Bado ni 0-0 hapa uwanjani timu zikishambuliana kwa zamu

43' Saidoo analisakama goli la Simba ila anaunawa inakuwa freekick

45' imeongezwa Dakika 1 kuelekea Halftime

Mpiraaa ni Halftime, Simba 0 Yanga 0

----------------------------------------

Kipindi cha pili kimeanza Simba 0 Yanga 0

45+1' Simba wanashambulia mara mbili hapa langoni mwa Yanga lakini golikipa Diara Djigui anakaa imara sana anaiweka Yanga salama


48' Yanga wanashambulia lango la Simba lakini Kapombe anakataa

52' Feitoto na Aucho wanaonana pale, wanampa Ntibazonkiza inakuwa Kona kwa Yanga.. Kona inaingizwa inaokolewa inakuwa kona Dotto..inaingizwa pale inaokolewa tena..


56' Yanga wanapanga shambulizi lakini Simba wanakataa kwa Tshabalala kukaa imara wakati huo Feitoto anapewa Kadi ya njano


59' Mpira unagonga mwamba hapa ulipigwa na Saido Ntibazonkiza.. Mayelee... Offside

62' Feisal yuko chini pale amechezewa faulo, madaktari wanakuja kumuangalia...Kibu Nje, Bwalya ndani

66' Bado ngoma ngumu 0-0 Wakati huo Yanga wanasakama lango la Simba ila shambulizi linadhibitiwa

71' Sub kwa Yanga Moloko out, Farid Ndani

73' Kona kwa Simbaa, inapigwa na Yanga inaenda juu nje pale

75' Kadi ya njano kwa Benard Morison

78' Simba washambulia Goli la yanga ila Mwamnyeto anaokoa pale inakuwa kona..

79' Bocco In, Morison out..Kona inapigwa na Bwalya inaenda nje pale baada ya Bocco kuigusa
Yusuf Mhilu anaingia, Kagere nje

84' Mayele out, Makambo In

86' Sadio kanoute anamchezea faulo Aucho pale

88' Simba wanafanya shamulizi hatari kupitia Kanoute lakini Bocco anakosa goli hapa..clear chance wakati huo Diara D yuko chini

90' Dakika 3 zinaongezwa kukamilisha Derby ya kariakoo

90+2' Simba wanawasakama Yanga ila mpira unatoka nje..Dilunga anatoa mpira nje

90+3' Manula anadaka anaanza mbele unaokolewa na mpira umeisha hapo

Watani wanagawana point moja moja
Yanga wanakuwa na point 20 wakiongoza ligi na Simba wakiwa nafasi ya pili na point 18

Ahsanteni kwa kuwa pamoja nami kwa updates hizi kwenye mechi hii ya kibabe ya mahasimu wa Kariakoo

FULL TIME SIMBA 0 - 0 YANGA
 
Naona mapema sana ila kitaeleweka [emoji617][emoji617]

20211208_172439.jpg
 
Back
Top Bottom