Nimeangalia mpira kwa umakini sana. Simba walikuwa wanapoteza mipira hovyo kuliko Yanga, hata kipindi cha pili Simba bado hawakufanya shambulizi lolote la maana golini kwa Yanga zaidi ya Shuti moja la Kanoute, nadhani watu wameona ameperform kisa tu kupiga shuti lile, ila katikati Simba hawakuwa vizuri na hata Kanuote amepoteza mipira mingi sana. Simba wamecheza rafu nyingi zaidi ya Yanga hii inaonesha ni jinsi gani walikuwa wanajihami dhidi ya mashambulizi.
Onyango amefanya kazi nzuri sana kwa kumdhibiti Mayele na sio INONGA.
Next game Simba isirudie makosa kuwaanzisha MORRISON, KIBU, DILUNGA NA KAGERE kwa pamoja, walikuwa mzigo mzito kwa viungo wakabaji wa Simba maana hawawezi kukaba pindi mpira unakuwa kwa YANGA.
Kwa ujumla mechi ilikuwa nzuri tena sana, refa kachezesha vizuri, makosa yaliyopo ni ya kibinadamu tu.