Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

TP Mazembe amechukua CAFCL mara tano.

Al ahly amechukua CAFCL mara 10...
Hilo neno Lina maana pana. Al Ahly ni timu ambayo tulishakutana nayo mara nyingi na tunawamudu. Na ili Al Ahly awe bingway hachezi na Simba tu anacheza na wengine pia.

Na Al Ahly kuwa bingwa mara kumi haiondoi ukweli kuwa tunammudu.

Al Ahly hawezi kuja kwa Mkapa kucheza na Utopolo akaja kwa wasi wasi sababu anajua Ni timu yenye viwango vya chini.

Al Ahly anakiri kuwa anaogopa viwanja vitatu Afrika 1.Kwa Mkapa-simba
2.Lubumbashi-Tp Mazembe
3.Na Mamelod -SA

Kwa soka la kimataifa Yanga ni timu ndogo Sana Afrika.
 
Yani Nyie Muwe Saizi Ya Al Ahly Au Zamakek Hv Huoni Aibu??, Haya Kwa Mpira Upi?? Au Kwa Pesa Zipi?? [emoji849]
Labda tu umeanza kushabikia mpira leo.

Al Ahly tulikuwa nae kundi moja MWAKA jana na tulimwongoza akaja nyuma yetu. Anatujua.

Hao hao zamalek wanaijua vzr Simba.

Hapa hatuongelei uchumi wa klabu bali performance ya mpira uwanjani. Ndiyo maana Mazuzu hamna akili.
 
Unajipa moyo tu ila kwa mpira huna cha ajabu umekimbizwa kama mtoto kipindi cha 2 ndo kdg umezinduka

Huyo Al ahly utamweza wap?
Nikazinduka wewe ukalala ukasali mechi iishe haraka.

Umesahau tu kwa uchache Al Ahly tulikuwa nae makundi klabu bingwa Africa mwaka jana. Anatujua vzr tumemuuzia na mchezaji coz Simba Ni klabu bora.

Pale utopoloni Al Ahly atamsajili nani. Kabwili?
 
One day jaribu kuchambua mpira kwa kuweka unazi pembeni mkuu

Naheshimu sana michango yako
Refa alijitahidi sana kubalansi ile mechi otherwise Utopolo angelala vizuri tu.

Refa yy ndiye anajua kwanini ilibidi afanye hivyo. Siri yake.
 
hilo neno Lina maana pana. Al Ahly ni timu ambayo tulishakutana nayo mara nyingi na tunawamudu. Na ili Al Ahly awe bingway hachezi na Simba tu anacheza na wengine pia...
Malmo FF ndo timu iliyocheza mechi nyingi na Real Madrid katika UEFACL.

Real Madrid ndo GOAT katika UEFACL kwa maana ana title 13.

Malmo FF hana title yoyote ya UEFACL.

Lakini FC Barcelona ana title 5 za UEFACL

FC Barcelona na Real Madrid hawajawi kukutana kabisa katika UEFACL.

Sasa kati ya Malmo FF na Barcelona Nani ana level sawa na Real Madrid?

Ukipata jibu relate na shudu uliyoiandika wewe MbuX3.
 
Malmo FF ndo timu iliyocheza mechi nyingi na Real Madrid katika UEFACL.

Real Madrid ndo GOAT katika UEFACL kwa maana ana title 13...
Mkuu acha fix Barca wamewahi kukutana na Real Madrid.

lionel_messi_scores_the_opening_goal_in_barcelona_s_2-0_victory.jpg
 
Labda tu umeanza kushabikia mpira leo.

Al Ahly tulikuwa nae kundi moja MWAKA jana na tulimwongoza akaja nyuma yetu. Anatujua..
Hiiii...!! We Kweli Popoma Sasa Nyie Mna Performance Gani Kuizidi National Al Ahly Si Mngekuwa Mabingwa Nyie Basi...Na Kwanza Mbona Mpo Shirikisho Huko?

Kama Nyie Level Sawa Na Izo Timu..Al Ahly Anaweza Kutolewa Kichoko Kama Nyie Na Timu Ya Ajabu Ajabu Ina Jina Gumu Kaa Gololi [emoji23]
 
Hiiii...!! We Kweli Popoma Sasa Nyie Mna Performance Gani Kuizidi National Al Ahly Si Mngekuwa Mabingwa Nyie Basi...Na Kwanza Mbona Mpo Shirikisho Huko? Kama Nyie Level Sawa Na Izo Timu..Al Ahly Anaweza Kutolewa Kichoko Kama Nyie Na Timu Ya Ajabu Ajabu Ina Jina Gumu Kaa Gololi [emoji23]
popoma niko shirikisho nyie wajanja mko Mapinduzi cup. Sluggish!
 
Malmo FF ndo timu iliyocheza mechi nyingi na Real Madrid katika UEFACL.

Real Madrid ndo GOAT katika UEFACL kwa maana ana title 13...
Unaruka ruka tu.

Narudia ongea mpaka utapike ulimi lakini Utopolo si level zetu. Kimataifa level zetu ni Al Ahly. Hao ndiyo saizi yetu wala hatuna hofu kukutana nao.

Najua hii kauli inawachoma sana. Kwasababu safari yenu ni ndefu sana kimataifa na hao wachezaji wenu wa mchongo Tena wachovu.

Pole Mkuu!
 
Hiiii...!! We Kweli Popoma Sasa Nyie Mna Performance Gani Kuizidi National Al Ahly Si Mngekuwa Mabingwa Nyie Basi...Na Kwanza Mbona Mpo Shirikisho Huko? Kama Nyie Level Sawa Na Izo Timu..Al Ahly Anaweza Kutolewa Kichoko Kama Nyie Na Timu Ya Ajabu Ajabu Ina Jina Gumu Kaa Gololi [emoji23]
mm sizungumzii ubingwa nazungumzia performance ya Simba dhidi ya timu kubwa km hizo.

Mbona hata la 3ujamaa akisoma ataelewa ninachoongea?

Acha Musukuma apate PhD tu kwasababu.
 
popoma niko shirikisho nyie wajanja mko Mapinduzi cup. Sluggish!
Mkuu hivi yule Bocco ndo Anafanya Mjitutumue Kiasi Hicho mpaka Kujifananisha na Level ambazo Hata Robo Hamjafika Ok!! ila Angalieni Tu Msijambe...
 
mm sizungumzii ubingwa nazungumzia performance ya Simba dhidi ya timu kubwa km hizo...
Mna Performance Gani Wewe JEHU, Usilete Stori Za Shangazi Yako...Sasa Si Mngekuwa Mnakuwa Mabingwa Nyinyi Kama Nyie Kweli Wa Level Moja....
 
Naaam wasalam,

Ile siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika..leo mtoto hatumwi dukani.

Karibuni katika matukio mubashara(live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa Soka la bongo, Simba na Yanga utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.

Huu ni mchezo wa ligi kuu ya NBC Simba akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Yanga.. mchezo uliopita sa ngao ya jamii Simba aliangukia pua kwa goli moja kwa sifuri kutoka kwa Yanga.

Pia Simba mechi ya mwisho kimashindano imetoka kupoteza 2_1 kutoka Red Arrows na hivyo kufuzu kwa aggregate ya 4-2 katika kombe la Shirikisho Afrika... Yanga ilicheza mechi ya mwisho ligi kuu na Mbeya Kwanza na kushinda 2_0.


Nani ataibuka kidedea, kaa nami hapa mwanzo kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa.

_____________________________________________________________
Updates zaidi kukujia kadiri zinavyopatikana.

>>Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni Hery Sassi na wasaidizi wake kama ilivyotangazwa awali

>>Azam Tv kupitia chaneli ya Azam sports 1 HD watakuwa mubashara (live).

-----------‐-------------------------------------------------
Kikosi cha Simba kinachoanza (STARTING XI)
1. Manula Aishi
2.Kapombe Shomary,
3. Hussein Mohamed ( Captain)
4. Onyango Joash
5. Inonga Henock
6.Mkude Jonas
7. Denis Kibu,
8. Kanoute Sadio,
9. Kagere Meddie,
10.Morrison Benard
11. Dilunga Hassan

Substitute(Akiba): B. Kakolanya, Israel P, Kennedy J, Erasto N, Mzamiru Y, P. Banda, Bocco J, R. Bwalya, Mhilu Y.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo (STARTING XI)
1.Djidgui Diarra
2.Djuma Shabani
3.Kibwana Shomary
4.Mwamnyeto Bakary (Nahodha)
5.Job Dickson
6.Bangala Yannick
7. Aucho Khalid
8.Moloko Jesus
9. Ntibazonkiza Saido
10. Feisal Salum
11. Mayele Fiston

Akiba /Substitute Johora Erick, Bryson David, Shaibu Abdalla, Yassin Mustafa, Mauya Zawadi, Makambo Heritier, Kaseke Deus , Yusuf Athuman, Farid Musa

------------------------------------------------------------------

Karibuni, muda mchache ujao kipute kinaanza hapa Dimba la Mkapa lililofurika mashabiki huku kukiwa na Magepu machache katika baadhi ya viti/majukwaa hapa

>> Timu ndio zinaingia uwanjani hapa kujipanga tayari kuanza soka

01' Mpira umeanza hapa kwa Kasi Yanga wakianza kusukuma gozi la ngombe kuelekea Simba

03' Fiston Mayele anakokota mpira kuelekea Simba ila anadhibitiwa anaanguka kwenye 18 ya simba

06' Yanga wanashambulia lango la Simba, Aishi Manula anachomoa mkwaju pale kutoka kwa Moloko..namna gani pale

08' Morison anacobtol mpira kifuani pale anapiga shuti inakuwa off target

11' Zimbwe anatoa mpira inakuwa kona ya kwanza kwa YANGA inapigwa na Saido Ntibazonkiza.. inapigwa pale inaookolewa na Kanoute..

12' anakokota Morison hadi nje ya box anaangushwa na Job D..

13' Faulu kwa Yanga Simba wanapiga kypitia Morison ila inaokolewa na ukuta mzuri wa yanga

14' Yanick anaangushwa na H Dilunga... Kasi ya mchezo ni kubwa huku wachezaji wakicheza kwa tahadhari

19' Morison anapiga shuti kuuubwa linaenda nje 0ale

22' Feisal anaangushwa inakuwa ni Faulu, inapigwa na Saidoo inaokolewa

24' Faulu kwa Yanga, Onyango njano kadi anapewa kwa kumzuia Mayele.. inapigwa pale aaaaa Aucho anapiga kichwa mpira unatoka nje

27' Yanga wanashtukiza hapa golini, Mayele anakosa control na mpira na kukosa goli hapa..aisee

31' Kapombe S. Yupo chini baada ya kukabana na Saidoo..wakati huo mpira uko nje.. Kapombe anapatiwa matibabu

34' Freekick kwa Yanga, Feisal a naangushwa wnaanza inaokolewa..mpira bado ni wa kasi

40' Bado ni 0-0 hapa uwanjani timu zikishambuliana kwa zamu

43' Saidoo analisakama goli la Simba ila anaunawa inakuwa freekick

45' imeongezwa Dakika 1 kuelekea Halftime

Mpiraaa ni Halftime, Simba 0 Yanga 0

----------------------------------------

Kipindi cha pili kimeanza Simba 0 Yanga 0

45+1' Simba wanashambulia mara mbili hapa langoni mwa Yanga lakini golikipa Diara Djigui anakaa imara sana anaiweka Yanga salama


48' Yanga wanashambulia lango la Simba lakini Kapombe anakataa

52' Feitoto na Aucho wanaonana pale, wanampa Ntibazonkiza inakuwa Kona kwa Yanga.. Kona inaingizwa inaokolewa inakuwa kona Dotto..inaingizwa pale inaokolewa tena..


56' Yanga wanapanga shambulizi lakini Simba wanakataa kwa Tshabalala kukaa imara wakati huo Feitoto anapewa Kadi ya njano


59' Mpira unagonga mwamba hapa ulipigwa na Saido Ntibazonkiza.. Mayelee... Offside

62' Feisal yuko chini pale amechezewa faulo, madaktari wanakuja kumuangalia...Kibu Nje, Bwalya ndani

66' Bado ngoma ngumu 0-0 Wakati huo Yanga wanasakama lango la Simba ila shambulizi linadhibitiwa

71' Sub kwa Yanga Moloko out, Farid Ndani

73' Kona kwa Simbaa, inapigwa na Yanga inaenda juu nje pale

75' Kadi ya njano kwa Benard Morison

78' Simba washambulia Goli la yanga ila Mwamnyeto anaokoa pale inakuwa kona..

79' Bocco In, Morison out..Kona inapigwa na Bwalya inaenda nje pale baada ya Bocco kuigusa
Yusuf Mhilu anaingia, Kagere nje

84' Mayele out, Makambo In

86' Sadio kanoute anamchezea faulo Aucho pale

88' Simba wanafanya shamulizi hatari kupitia Kanoute lakini Bocco anakosa goli hapa..clear chance wakati huo Diara D yuko chini

90' Dakika 3 zinaongezwa kukamilisha Derby ya kariakoo

90+2' Simba wanawasakama Yanga ila mpira unatoka nje..Dilunga anatoa mpira nje

90+3' Manula anadaka anaanza mbele unaokolewa na mpira umeisha hapo

Watani wanagawana point moja moja
Yanga wanakuwa na point 20 wakiongoza ligi na Simba wakiwa nafasi ya pili na point 18

Ahsanteni kwa kuwa pamoja nami kwa updates hizi kwenye mechi hii ya kibabe ya mahasimu wa Kariakoo

FULL TIME SIMBA 0 - 0 YANGA
..
 
Back
Top Bottom