Ligi kuu Tanzania Bara kuendelea Leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wanaenda kukutana na Wajelajela walohamishia makazi yao Sumbawanga wakitokea Mbeya
Ikumbukwe ni match ya kulipa kisasi kwa simba ambao walipoteza match yao ya kwanza kwenye uwanja wa Nelson Mandela na ni muhimu kwa Simba kwani ushindi utawafanya kumsogelea Dar Young Africa ambae ana point hamsini na simba ana arobaini na tano
Wajela jela ni wataalam wa kutoa draw lakini naona kila dalili ya wao kupoteza dhidi ya mnyama anaetaka kulipa kisasi
Kaa hapa hapa kwa ajili ya updates za mchezo huu na ikumbukwe match ni saa 1 kamili usiku.
=======
00' Mwamuzi kashapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa kusukuma gozi
18' Luis anajaribu nje ya 18 lakini inakuwa off target
26' Simba wanapata penati baada Medatus kuunawa ndani ya 18
28' Mugalu anapiga mkwaju wa penati na Jeremiah anaupangua, Simba 0-0 Prisons
42' Kadi nyekundu kwa Jumanne Elfadhil baada ya kuokoa mpira na mguu wake kushukia shingoni kwa Mzamiru Yassin.
45' Mlinda mlango wa Tanzania Prisons, Kisubi yuko chini
45+3' Kisubi anainuka lakini Free kick ya Luis inagonga ukuta
45+6' Mpira Mapumziko