Simba SC 1-1 Tanzania Prisons | Mkapa Stadium | VPL

Simba SC 1-1 Tanzania Prisons | Mkapa Stadium | VPL

Ligi kuu Tanzania Bara kuendelea Leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wanaenda kukutana na Wajelajela walohamishia makazi yao Sumbawanga wakitokea Mbeya

Ikumbukwe ni match ya kulipa kisasi kwa simba ambao walipoteza match yao ya kwanza kwenye uwanja wa Nelson Mandela na ni muhimu kwa Simba kwani ushindi utawafanya kumsogelea Dar Young Africa ambae ana point hamsini na simba ana arobaini na tano

Wajela jela ni wataalam wa kutoa draw lakini naona kila dalili ya wao kupoteza dhidi ya mnyama anaetaka kulipa kisasi

Kaa hapa hapa kwa ajili ya updates za mchezo huu na ikumbukwe match ni saa 1 kamili usiku.

=======

00' Mwamuzi kashapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa kusukuma gozi

18' Luis anajaribu nje ya 18 lakini inakuwa off target

26' Simba wanapata penati baada Medatus kuunawa ndani ya 18

28' Mugalu anapiga mkwaju wa penati na Jeremiah anaupangua, Simba 0-0 Prisons

42' Kadi nyekundu kwa Jumanne Elfadhil baada ya kuokoa mpira na mguu wake kushukia shingoni kwa Mzamiru Yassin.

45' Mlinda mlango wa Tanzania Prisons, Kisubi yuko chini

45+3' Kisubi anainuka lakini Free kick ya Luis inagonga ukuta

45+6' Mpira Mapumziko
Prisons Wamepania Sana, mpira haujatulia kwao. Watafungwa
 
Kila heri mnyama mkali
Piga hao wajela jela
 
Penalty
Red Card
In 45'

Hii ndo inaitwa utake usitake utashinda tu
 
Simba sasa waamke. Lakini wachukue tahadhari maana wachezaji wataumizwa sana.
 
Itakuwa suala la aibu kufungwa na prisons nje ndani
 
Back
Top Bottom