Simba SC 2 - 1 Yanga SC: Shiza Kichuya aibuka shujaa wa Simba

Simba SC 2 - 1 Yanga SC: Shiza Kichuya aibuka shujaa wa Simba

Kivipi na unaona updates kwa matukio yote muhimu?au unadhani nipo dimbani unaniuliza mbona sifungi?
Na bado mtaita maji mma leo, time will tell. Oooh by the way hongera mtani, upo mpaka muda huu, maajabu basi Yanga washindi leo. Bundi kakaa katikati ya uwanja.
 
Na bado mtaita maji mma leo, time will tell. Oooh by the way hongera mtani, upo mpaka muda huu, maajabu basi Yanga washindi leo. Bundi kakaa katikati ya uwanja.
Tulia binti kwani dakika ya ngapi,au huko kwenu mpira umeisha?
 
e8e1f1986421c5afbb84481e6f92bf21.jpg
3e2bc465fbae6494f8702b8dc15e87ef.jpg
Eee bhana huo ni uchaguzi wa Marudio Zanzibar au ni soka ?
 
Simba wako pungufu na sub washamaliza. Hatari sana hii.

Inabidi tuongeze jingine. Haraka sana
 
Ndugu wanajukwaa kama mnavyofahamu ile siku mahsusi ya mechi kali kati ya derby wa Tanzania Simba SC na Yanga SC ni leo. Timu hizi licha ya kuwa ni watani wa jadi na zenye mashabiki wengi kuliko timu derby zozote Africa mashariki, zinachuana vikali kutafuta ubingwa zikitofautiana kwa alama moja

Mechi itapigwa katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10 jioni. Mechi hii itarushwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV. TBC1 nayo itarusha moja kwa moja matangazo ya Radio. Jamiiforums nayo haitakuwa nyuma itakuletea moja kwa moja kutoka uwanja wa Taifa

Hatujafanikiwa kupata jina la mgeni rasmi wa mechi hii, lakini habari zilizotufikia ni kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowasa, Mwenyekiti Mh.Mbowe, Waziri wa Ndani Mh.Mwigulu Nchemba, Major wa Ubungo Mh.Jacob, Mrembo wa Tanzania 2006 Mh.Wema Sepetu, watakuwepo uwanjani

Mkuu wenu nitawaletea moja kwa moja mechi hii hapa hapa JF, usiondoke



Updates

DK 1. Mpira umeanza

DK 3: Yanga wanapata penati baada ya Chirwa kuangushwa na mlinzi wa Simba eneo la Penati.

DK 4: Mathew Akrama anamlamba kadi ya njano Lufunga kwa kumuangusha Chirwa

DK 5 - Goal: Simon Msuva anawaandikia Yanga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati.

DK 10: Simba wanaonesha kumiliki mpira, Yanga wanakuwa makini.

DK 13: Mavugo anapokea pasi nzuri lakini anakuwa butu na kupoteza mpira ule muhimu langoni mwa Yanga, Dida anaudaka.

DK 15: Mchezo sasa upo balanced huku mipango ya Simba ikiwa haijakaa vizuri, wanashindwa kujiamini.

DK 16: Juma Luizio anaotea.

DK 17: Simba wanafanya mashambulizi lakini Dida anawahi na kudaka, Yondani yupo chini baada ya kugongwa katika purukushani hiyo.

DK 19: Kamusoko anapiga krosi murua kutokea kulia, Chirwa anaunganisha kwa kichwa na Agyei anadaka.

DK 20: Yanga wanafanya shambulizi lakini Niyonzima anapiga shuti la kitoto Agyei anaudaka.

DK 22: Kotei anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni kwa Msuva

DK 23: Krosi safi ya Juma Abdul, Zimbwe anaokoa na kuwa kona ya kwanza

DK 23: Niyonzima anachonga kona nzuri hapa lakini Agyei anaruka na kupangua

DK 25: Kamusoko anapokea pasi murua kutoka kwa Chirwa, anapiga shuti lakini mpira haujai vizuri mguu hivyo kuwa dhaifu, Agyei anaudaka.

DK 26 - Sub: Simba wanafanya mabadiliko ya mapema, Anaingia Ndemla na kutoka Luizio.

DK 28: Zuru anapoteza pasi muhimu sana ambayo ingewapa Yanga goli la pili muhimu

DK 29: Nafasi nzuri zaidi kwa Simba, Mavugo akiwa amebaki yeye peke yake na kipa Dida, anapiga mpira wa kichwa dhaifu na unatoka nje.

DK 32: Mavugo anawachambua kama karanga mabeki wa Yanga, Yondani anazuia shuti la Mavugo na Munishi anaudaka.

DK 34: Munishi analeta mbwembwe baada ya kudaka mpira baada ya kukaa na mpira mkononi kwa zaidi ya muda unaoruhusiwa. Simba wanapiga mpira wa adhabu ndogo ndani ya eneo la 18.

DK 35: Said Mdemla anapiga shuti linapaa aka mnazi.

DK 37: Yanga wanafanya shambulizi lakini Agyei anauwahi mpira. Ndemla anapiga shuti maridadi lakini linatoka nje ya lango la goli.

DK 40: Mo Ibrahim anaachia shuti kali sana lakini Munishi anaupoza mpira kwanza na kuudaka.

DK 41: Simba wanaonekana kuzinduka wakati huu wa kuelekea mapumziko. Wanapiga moja mbili lakini Dida anaudaka mpira.

DK 42: Kamusoko anapiga shuti tena lakini mpira haujai mguu, mpira unatoka nje na kuwa goal kick

DK 42: Kamusoko yuko chini baada ya kugongana na Muzamiru

DK 44: Mo Ibrahim analazwa chini karibu na eneo la boksi, anajirusha hadi kwenye 18, wachezaji wa Simba wanadai penati ila refa anasema ni kwenye ukingo wa boksi.

DK 45: Hajibu anapiga mpira wa adhabu, inakuwa goli kick.

DK 45+1: Kamusoko anaonekana hali yake haijatengamaa, analala chini na refa anaita huduma ya kwanza na kumtoa nje ya uwanja

DK 45+3 - Sub: Kamusoko anatoka, anaingia Said Juma Makapu

DK 45+4: Mpira ni mapumzikooooooooo

DK 46: Mpambano wa mahasimu unarejea tena kipindi cha Pili huku Yanga wakiwa kifua mbele kwa bao moja la Msuva.

DK 46: Simba wanafanya mashambulizi ya mfululizo mara mbili lakini umakini wa Munishi anaweza kuokoa hatari zote.

DK 48: Simba wanafanya mashambulizi karibu kabisa na lango la Yanga, Mavugo anamfanyia madhambi mchezaji wa Yanga.

DK 50 -SUB: Anatoka Lufunga anaingia Shiza Kichuya.

DK 52: Mavugo anachezewa madhambi, refa anampa kadi ya njano Vincent wa Yanga

Dk 53: Banda analazimika kufanya kazi ya ziada na kuwa kona
KADI Dk 52, Vicent analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Mavugo

Dk 53: Msuva anageuka vizuri kwenye boksi la Simba na kuachia mkwaju mkali kabisa, GOAL KICK

DK 55- Red Card: Boukungu anamuangusha Chirwa akiwa amebaki peke yake nje ya eneo la hatari, anatolewa nje kwa kadi nyekundu

DK 56: Anapiga faulu nzuri lakini Agyei anauona mpira na kuudaka.

DK 57: Simba wanafanya shambuli na kupata kona, Kichuya anaenda kuchonga kona.

DK 57- SUB: Simba wanamtoa Mo Ibrahim na nafasi yake inachukuliwa na Jonas Mkude

DK 63: Yanga wanafanya shambulizi lakini Agyei anatokea na kuondosha hatari

DK 64: Hajibu anapiga shuti kimo cha sungura na Munishi anaudaka kwa umaridadi

7c76901338b1e4b63d010e92ecd75443.jpg
 
Back
Top Bottom