Simba SC 3-0 JKT Tanzania FC | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu, Vodacom Premier League VPL' kuvurumishwa leo Machi 1, 2021 ambapo Mnyama Mkali, Simba SC wanapambana na JKT Tanzania FC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huu inatarajiwa kuwa kali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu ikiwania kusaka ushindi wa alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo wa VPL.

Kwenye mchezo uliofanyika 4, 10, 2020 JK Tanzania walilala kwa jumla ya mabao nne kwa bila. Je leo JKT Tanzania watakubali kuwa wateja kwa Mnyama Mkali kwa mara nyingine?

Usikose Ukasimuliwa.. Kumbuka mtanange huu wa VPL ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.
============

00' Naaaam mpira umeanza uwanja wa Benjamin Mkapa.

08' Chris Mugalu anaipatia Simba SC bao la kwanza, baada ya krosiiiiiiii kutoka kwa Miquissone

37' Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Nyoni.

Mpira ni mapumziko, Simba SC wapo mbele kwa mabao mawili kwa bila.

45+1' HT, VPL Simba SC 2-0 JKT Tanzania

Kipindi cha pili kimeanza kwa JKT Tanzania kutaka kujaribu kusawazisha makosa ya kipindi cha kwanza.

Umiliki wa Simba SC sasa. Kutafuta bao la tatu.

90+3' John Bocco anaipatia Simba SC bao la tatu akipokea pasi safi kutoka kwa Bwalya

FT, VPL Simba SC 3-0 JKT Tanzania





 
Naaam nakupata kwa uzuri kabisa nikiwa na represent kutoka upande wa juu

upande wa mbali, upande uliowekwa na asili yetu,.

upande wenye uthubutu na maamuzi, upande ambao pengine kuishi shabiki wa YANGA ni ngumu

upande ambao haushabikii tija Kama hauamini pima, utagundua upande ilipo SIMBA ni ngao ya jamii nzima
 
Vikosi vyote vipo uwanjani vipipasha misuli moto kijiweka tayari kwa mchezo huu wa VPL

Simba SC Vs JKT Tanzania
 
Paka fc bila mbeleko ni wepesi kama unyoya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…