Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nguvu moja.. 💪🏻💪🏻Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CAF Confedaration Cup, Simba Sc itashuka dimbani dhidi ya Us Gendarmerie katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 4:00 usiku.
Hiyo itakuwa mechi ya mwisho ya kundi D na Simba wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kufuzu hatua ya robo fainali.
Endapo Simba itashinda watafuzu kwa hatua ya robo fainali huku pia wakisikilizia matokeo ya Rs Berkane Vs Asec Mimosas mechi ambayo nayo itapigwa saa 4:00 usiku Kwa saa za Afrika ya Mashariki.
Hii itakuwa mara ya kwanza Simba kucheza mechi saa 4:00 usiku jambo ambalo linatia mashaka kama mashabiki watajitokeza kwa wingi kulinganisha na hali ya usalama.
Je Simba wataweza kufuzu robo fainali? Majibu ni saa 4:00 usiku kupitia ZBC2
Umeandaa popcorn bebii?Kila la kheri Simba Fc [emoji91]
Hela ndogo sana hiyo...africa unasafiri kote alafu hela yenyewe ni hiyo....Simba akivuka hatua hii anaingiza $350,000 kibindoni
Ni wivu tuuHela ndogo sana hiyo...africa unasafiri kote alafu hela yenyewe ni hiyo....
Ndio maana wasenegal wana akili sana baadala ya kupoteza hela kisafiri africa nzima bora hela unayotumia uweke kwenye academy uuze wachezaji ulaya.
Kumbuka kila hatua unayopiga ni mpunga tu.Hela ndogo sana hiyo...africa unasafiri kote alafu hela yenyewe ni hiyo....
Ndio maana wasenegal wana akili sana baadala ya kupoteza hela kisafiri africa nzima bora hela unayotumia uweke kwenye academy uuze wachezaji ulaya.
Ki black Russia shng ngapi!?Simba akivuka hatua hii anaingiza $350,000 kibindoni
Sio wivu ndio ukweli huo. Wee ulishaona timu za senegal kwenye haya mashindano ya caf wakifika mbali?Ni wivu tuu
Ndio nalijua hilo but prize money ni ndogo ukilinganisha na gharama unazotumia....Kumbuka kila hatua unayopiga ni mpunga tu.
Ndio maana hata nyie Yanga huwa hampendi kufika mbali kwenye haya mashindano maana hayana pesaSio wivu ndio ukweli huo. Wee ulishaona timu za senegal kwenye haya mashindano ya caf wakifika mbali?
Ila wao wanapelela wachezaji ulaya of which wnawez uza for ova one million usd...plus kuna percent wanaendelea kupata endapo mchezaji atakuwa anaenda another club.
Nakuja nazo mrembo,andaa Siti ya wawiliPopcorn zinanoga kwenye match Kali kama hii .
Usisahau refreshing drinks