Simba SC ama mzishtaki hizi Timu au muendelee Kunyamaza ili Shutuma hizi zizidi Kuaminika na 'Brand' yenu Kuchafuliwa

Simba SC ama mzishtaki hizi Timu au muendelee Kunyamaza ili Shutuma hizi zizidi Kuaminika na 'Brand' yenu Kuchafuliwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sasa hapa nchini Tanzania imekuwa ni kawaida Timu yoyote ile ya VPL ikija kucheza na Simba SC uwanja wa Mkapa na ikifingwa tu Kihalali (Kimchezo) itasingizia kuwa walipuliziwa Dawa Vyumbani.

Upuuzi huu waliuanza Timu ya Azam FC na baadae tena wakaja nao Namungo FC, kisha Kagera Sugar FC na hatimaye baada ya Dodoma Jiji FC Kufungwa 'Kimchezo' kabisa jana na Simba SC goli 3 kwa 0 sasa wameamua kuiachia ' Video Clip ' wakionyesha kuwa katika ' Dressing Room ' yao Kulipuliziwa Dawa ya Kuwamaliza nguvu.

Nina Maswali yangu kadhaa tu...

1. Je, Dodoma Jiji FC wangeshinda jana hiyo Video yao wangeiachia?

2. Kama walikuwa wanaamini hivyo je, ni kwanini hawakuiachia hiyo Video kabla ya Mechi kuanza?

3. Kisheria Timu zote hukabidhiwa Vyumba vyao Masaa Saba mpaka hata Kumi kabla ya Mechi kuanza ili Kuvilinda je, hiyo Dawa ilimwagwa na nani humo Vyumbani wakati Wadhibiti wa Chumba chao walikuwa ni Wao wenyewe?

4. Je, Timu inayopuliziwa Dawa Daktari wake (wao) anaweza kuiruhusu iingie tena humo Vyumbani?

5. Je, Timu inayopuliziwa Dawa Vyumbani kama Dodoma Jiji FC ingeweza Kucheza mpira ule mkubwa na kuleta Upinzani japo tunaoujua Mpira tunajua kuwa Dodoma Jiji FC jana walizidiwa tu Kiuwezo na Kiufundi na Timu bora ya Simba SC?

6. Je, na katika Mechi zingine Mbili ambazo Dodoma Jiji FC alizokutana na Simba SC na Kufungwa (ikiwemo ya Kucheza Kwao Mkoani Dodoma) Simba SC waliwapulizia Dawa Vyumbani mwao?

7. Kama walishajua kuwa Vyumbani mwao wamepulizuwa Dawa na Simba SC je, ni kwanini hadi Alfajiri hii GENTAMYCINE naandika Uzi huu hakuna sehemu yoyote ile Dodoma Jiji FC wamepeleka Barua ya Kulilalamikia hili na badala yake wamekimbilia tu humu Mitandaoni kuachia hiyo 'Video Clip' yao wakimwaga Maji Vyumbani ili ' Kuikata ' hiyo harufu?

Labda leo niwaambie Dodoma Jiji FC kuwa GENTAMYCINE nipo katika Mpira wa Tanzania Kitambo na ninachojua tu ni kwamba karibia 99% ya Viongozi Waandamizi wa Dodoma Jiji FC ni Mashabiki na Wanachama wakubwa wa Yanga SC wakiongozwa na Mbunge wao Antony Mavunde na Kiongozi Mmoja Mnafiki na Mfitini aitwae Kunambi.

Dodoma Jiji FC kwakuwa mmetuchokoza sasa mtuvumilie kwani nina Siri yenu moja kubwa ya Upangaji wa Matokeo (Match Fixing) mliifanya majuzi tu mlipocheza na Ihefu FC ambapo Wachezaji wenu walirushiwa Pesa katika Simu zao ili wacheze chini ya Kiwango Ihefu FC ishinde na kweli mliwaachia na mkafungwa.

Nina Rafiki yangu mkubwa sana yupo katika Timu ya Ihefu FC na hasa hasa katika Benchi la Ufundi na kuna Mchezaji wenu Mmoja ( tena Mshambuliaji ) Dodoma Jiji FC namlinda kwa Kutomtaja kwakuwa aliniomba sana wote Wawili hawa wamenithibitishia kuwa Mchezo huo Mchafu ulifanyika na unaendelea Kufanyika vile vile Kipindi hiki Ligi Kuu ya VPL ikielekea ukingoni.

Mlichoamua kukifanya Dodoma Jiji FC ni kuingia katika Mtego wa kutumika na Yanga SC katika ' Kuichafua ' Simba SC ili sasa Tanzania nzima na hata nje ya Tanzania ijulikane kuwa Simba SC inashinda na inabeba Vikombe mfululizo kwa Kuwapulizia Dawa Vyumbani Timu Pinzani.

Dodoma Jiji FC tafadhali GENTAMYCINE nawatumeni nendeni kwa hao 'Mabwana' zenu mnaowapenda Yanga SC na muwaulize je, na Wao wanavyofungwa mfululizo (tena Magoli mengi tu na Simba SC) kuanzia 6 - 0 Kipindi cha akina Kibaden, 4 - 0 Kipindi cha akina Machupa, 4 - 0 Kipindi cha akina Mgosi, 5 - 0 Kipindi cha akina Okwi na 4 - 1 Kipindi hiki cha akina Chama Simba SC ilikuwa inawafunga hivyo kwa Kuwapulizia Dawa hizo Vyumbani?

Sasa GENTAMYCINE narudi kwa Timu yangu pendwa ya Simba SC na hapa pia nitakuwa Mkali sana Kwenu na mnivumilie tu kwani nanyi kuna sehemu huwa mnanikwaza sana tu.

Uongozi wa Klabu ya Simba SC hii siyo mara ya Kwanza nyie 'Kushutumiwa ' na hata' Kuhusishwa 'na' Upuuzi ' huu. Ni kwanini huwa mnaunyamazia hadi sasa unaanza Kuaminika Masikioni mwa Watu (Wadau wa Soka) nchini?

Hivi Uongozi wa Simba SC mnajua kuwa mmetumia Nguvu kubwa sana Kuijenga ' Brand ' ya Simba SC na sasa Kukubalika ila kuacha hizi ' Shutuma ' zizidi Kuzoeleka na hata Kuaminika na Jamii ni Kuichafua ' Brand ' ya Simba SC ndani na nje ya Tanzania?

Uongozi wa Simba SC ni nini kinawazuia Kukemea 'Kuchafuliwa' Kwenu huku mara kwa mara na Timu Pinzani na hata ikiwezekana ' mkazishtaki ' ili zihukumiwe na liwe Fundisho kwa 'Wapuuzi' wengine?

Hivi Timu ya Simba SC haina Mawanasheria wake Mbobezi? Yeye hizi 'Shutuma' za kila Siku anaona ni sawa kwa Timu ya Simba SC? Huyu (huyo) Mwanasheria wa Simba SC ana Uchungu kweli na Simba SC yake kama nilionao Mimi GENTAMYCINE na naacha Usingizi wangu kuja Kulilalamikia na kulitolea Ufafanuzi Jambo hili ambalo Kitaswira linaichafua zaidi Simba SC yetu?

Je, Uongozi wa Simba SC tukihisi kuwa huenda Kukaa Kwenu Kimya hivi na Kuogopa kuchukua Hatua za Kisheria dhidi ya hizo ( hizi ) Timu zinazolalamika Kupuliziwa Dawa Vyumbani pengine ni Kweli huwa mnayafanya haya tutakuwa tunakosea au tunawaonea?

Msemaji wenu (wetu) Haji Manara haya ndiyo mambo ambayo 'Professionally' nadhani angekuwa nayo ' busy ' kuyaongelea, kuyakemea na hata kuilinda ' Brand ' ya Simba SC lakini cha Kushangaza na Kusikitisha Yeye kila Uchao tu ni ' Kuinanga ' Yanga SC huku katika Kurasa zake za Mitandao Kazi yake ni ' Kujisifu ' tu ' Upuuzi ' na ' Ushamba ' wake wa Kizaramo badala ya Kufanya Mambo ya maana, makubwa na yenye Tija na Maendeleo hasa kwa Idara Muhimu anayoiongoza.

Mara kwa mara Masikini ya Mungu GENTAMYCINE nimekuwa nikipiga sana Kelele hapa jinsi Mtangazaji Maulid Kitenge na Kipindi chake cha Michezo cha Sports Arena wanavyoiandama Simba SC kwa kwa Kuizushia na Kuichafua hadi Kuifitinisha Klabu kwa Kutumiwa na Yanga SC cha Kushangaza Msemaji wa Simba SC Haji Manara anakutana na Maulid Kitenge na Kuchekeana, Kula na Kunywa pamoja kisha baadae utaona Manara anasema kuwa Wamemalizana na Amani Iendelee. Kama huu siyo Unafiki ni nini?

Uongozi wa Simba SC kwa ' Upumbavu ' wenu na Kukaa Kimya ( Kunyamaza ) kwenu huku kwa Kuzushiwa Matukio mabaya ya Kimchezo na Kuandamwa ' Kunangwa ' na akina Kitenge na Wachambuzi mbalimbali nchini kutatufanya sasa na Sisi akina GENTAMYCINE tunaojua ( kuyajua ) mengi, wenye Uchungu na Timu, Kuipigania na Kuipenda pengine zaidi ya nyie huko Uongizini na huyo Manara wenu tukaamua Kunyamaza kimoja na kutojishughulisha kwa lolote lile la Kimaendeleo kwa Klabu yetu. Kiukweli inachosha na Kukera sana tu.

Tafadhalini Uongozi wa Simba SC naomba baada ya Kusoma Uzi wangu tu huu Mimi GENTAMYCINE nione mnaanza Kuyafanyia Kazi yote niliyoyaongelea hapa na ikibidi Mkono wa Sheria uhusike upesi katika ' Kuwashtaki ' hawa Wahuni kwani tumewachoka sasa na imetosha.

Na nyie TFF (hasa Wewe Tumbo Tumbo Rais Wallace Karia) endeleeni tu Kuyanyamazia haya mkidhani kuwa ' Kashfa ' zinaiathiri tu Simba SC wakati Kiukubwa hapq hata nyie mnaingia katika ' Doa ' kubwa la Kuonekana kuwa mnaongoza na kusimamia Ligi Kuu yenya ' Uhuni ' mwingi hivyo Kuwaathiri hadi katika kupata ' Wadhamini ' wa maana wa kuja Kuwekeza ' heavily ' katika Soka la Tanzania.

Simba SC chokeni sasa Kuchafuliwa tu.

OMBI
Tafadhali wale Wadau wangu wa Simba SC mlio karibu (jirani) na Mwekezaji Mohammed Dewji, CEO Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu, Mshauri Mkuu wa Mwekezaji na Ufundi Crescetius Magori na Msemaji wa Simba SC Haji Manara nisaidieni Kuutuma (Kuufowadi) huu Uzi wangu Muhimu mno Kwao ili wayafanyie Kazi yale yote niliyoyasema hapa. Nitawashukuruni sana Wadau.
 
Simba haisimamii viwanja.

Hiyo ni kazi ya Waandaa Matamasha iwe VPL, FA, Mapinduzi, CAFCL, CAFCC
 
Hao ni wafamaji hawaishi kutapa tapa, kuna watu ni ngumu sana kwao kukubali Simba ni bora kuliko wao lazima waje na kisingizio tu.
 
Simba haisimamii viwanja.

Hiyo ni kazi ya Waandaa Matamasha iwe VPL, FA, Mapinduzi, CAFCL,CAFCC
Huu Uzi nadhani kwa IQ yako ndogo ni Mzito Kuuelewa hivyo nakuomba wapishe Watu wenye Akili Kubwa na walionielewa Waujadili kwa marefu na mapana.

Labda kwa Akili ndogo tu nikuulize unadhani hao Dodoma Jiji FC hawajui nani Msimamizi wa Viwanja na Ligi? Na je, kama hawa ( hao ) uliowataja hapa ndiyo Wasimamizi wa Viwanja inakuwaje Siku moja kabla ya Mechi husika au Siku ya Mechi Timu zote Mbili hukabidhiwa Funguo za Vyumba vyao ili Wavilinde wao Wenyewe?

Ina maana kwa kutumia Akili yako ndogo tu umeshindwa kujua ' intetion ' Kuu ya Dodoma Jiji FC katika Kuiachia hiyo ' Video Clip ' baada ya Mechi yao na Simba SC jana Usiku waliyofungwa Goli 3 kwa 0 ni nini?

Usinilazimishe tu nikaanza Kukudharau.
 
Hao ni wafamaji hawaishi kutapa tapa, kuna watu ni ngumu sana kwao kukubali Simba ni bora kuliko wao lazima waje na kisingizio tu.
Juzi kuna Kiongozi Mmoja wa Yanga SC ( aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu ) katika Ukurasa wake wa Instagram namnukuu..." Kiukweli Kiutani huwa tunapenda Kuwatania Simba SC lakini Kiuhalisia haya Mafanikio makubwa ya Simba SC hasa Uwanjani ni Somo pia Kwetu Yanga SC na nikiri kuwa kwa sasa Simba SC ipo vizuri na hata Sisi Yanga SC tunapoenda kukutana nao tujiandae vilivyo " alimaliza.

GENTAMYCINE nabahatika sana Kukaa na hata kukutana na wana Yanga SC wanaojielewa na hata baadhi ya Viongozi wao Waandamizi wa sasa na waliopita ambao wamekiri kuwa kwa Tanzania Simba SC ipo vizuri Kiufundi ( Kiuchezaji ) na ukikutana nayo unatakiwa Kujipanga na Kujiandaa kiukweli ukweli.
 
Yanga SC yako wanavyofungwa mara kwa mara na Simba SC huwa wanasema nao wamepuliziwa Dawa Vyumbani mwao? You must be an authentic Moron on Earth.
Rudia kusoma nlicho andika, usikurukupuke au ume andika uzi kila mtu afuate mawazo yako?
 
Tuhuma za kupulizwa dawa kwenye vyumba haija anza leo, timu za nje na timu za ndani zimekua zikilalamika, meneja wa uwanja anatakiwa atolee ufafanuzi kwakua timu zikiwa zinatoa malalamiko yeye uwa ana shuhudia Sasa uwa anachukua hatuagani? Maana lazima meneja aonyeshwe Hali ya chumba husika Sasa akiwa ana kaa kimya inatia Shaka.
 
Huu Uzi nadhani kwa IQ yako ndogo ni Mzito Kuuelewa hivyo nakuomba wapishe Watu wenye Akili Kubwa na walionielewa Waujadili kwa marefu na mapana.

Labda kwa Akili ndogo tu nikuulize unadhani hao Dodoma Jiji FC hawajui nani Msimamizi wa Viwanja na Ligi? Na je, kama hawa ( hao ) uliowataja hapa ndiyo Wasimamizi wa Viwanja inakuwaje Siku moja kabla ya Mechi husika au Siku ya Mechi Timu zote Mbili hukabidhiwa Funguo za Vyumba vyao ili Wavilinde wao Wenyewe?

Ina maana kwa kutumia Akili yako ndogo tu umeshindwa kujua ' intetion ' Kuu ya Dodoma Jiji FC katika Kuiachia hiyo ' Video Clip ' baada ya Mechi yao na Simba SC jana Usiku waliyofungwa Goli 3 kwa 0 ni nini?

Usinilazimishe tu nikaanza Kukudharau.
Genta, wewe ni shabiki au mwanachama?
Naona umepaniki Sana
Kama ni mwanachama halali wa ssc unaweza kwenda mwenyewe mahakamani kufungua jalada la kesi. NI USHAURI TU
 
Hiyo clip imesambazwa hata kabla ya game kuanza nusura dodoma wasusie mechi
 
Mikia bila kupuliza viuatilifu hamshindi game,Ndumba F.C a.k.a Wazee wa kupindua Meza[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
20210523_073951.jpg
 
Back
Top Bottom