Simba SC haimtendei haki beki wa kimataifa, Mohammed Ouatara

Simba SC haimtendei haki beki wa kimataifa, Mohammed Ouatara

Niliona kuna maelezo fulani hapo juu uliandika na uliyafuta! Halafu na yeye aka ku quote! Anyway, lengo langu siyo kujiingiza kwenye mgogoro.

Pole sana. Jamii forums kuna wakati inakera dana. Hivyo huna budi kuichukulia.
Sijafuta kitu chochote mkuu maybe JF wamefuta. Jf wanafuta contents wanazoamua wao
 
Inashangaza sana mara baada ya beki aliyeisha makali yake, Joash Onyango kupeleka ombi la uhamisho kwa uongozi wa Klabu ya Simba, mambo yakaanza kubadilika kwa beki gwiji raia wa Ivory Coast Mohammed Ouatara, akaanza kusugulishwa benchi mfululizo.

Yaani toka kocha "Mzawa" Juma Mgunda atue Msimbazi, nafasi pekee anayoipata beki huyu imekuwa ni kukaa benchi tu. Huwa najiuliza, huyu beki Onyango anaogopwa pale Simba SC ama vipi?

Binafsi nikimlinganisha Ouatara dhidi ya Onyango naona kabisa Ouatara ni beki anayemzidi Onyango kwa mambo mengi mno. Kifupi jamaa ni beki haswa na combination yake na Inonga ilikuwa nzuri sana. Cha ajabu ni kuwa huyu Kocha Mgunda amekuwa akimpa nafasi ya nne katika chaguo lake la mabeki.

Hivi Onyango na Kennedy Juma wana nini cha kumzidi Momo Ouatara? Tuwe wa kweli, leo hii akija kocha yeyote kutoka nje anayejua mpira lazima atampa nafasi Ouatara dhidi ya hawa mabeki ambao wana spidi ya kobe na hawana hata udhibiti wa mpira achilia mbali kupiga tu pasi kuwa ni mtihani kwao.

Mgunda unajichongea kaburi lako mwenyewe kwa kuendekeza "Uzawa".
Kama haujui tu kuwa Outtara katokea Burkina Faso na siyo Ivory coast ni wazi kuwa hujawahi kumuona akicheza zaidi ya akiwa Simba. Kwa hiyo uliyoandika ni ya kupuuza tu.
 
Sasa mnashangaa nini na nyie?watoto wa nyumba moja wanagombana itakuwa mashabiki?.naona baadhi ya Utopolo msio na hoja ya kujenga sasa mmepata pa kusemea
 
Hao wote wametukanana! Hivyo wanatakiwa kubadilika. Ni bora tukaendela na huu utani wetu wa kawaida.

Matusi hayana tija hata kidogo kwa watu wazima. Halafu eti chanzo ni utani tu wa Yanga na simba!
Kwanza Mods wasipo wapiga ban nitajua kua sikuhuzi JF imeshuka hadhi.

Huyo Sister KALPANA mara nyingi comments zake kama anatangaza biashara flani kinguvuuu!!!!
 
Kwanza Mods wasipo wapiga ban nitajua kua sikuhuzi JF imeshuka hadhi.

Huyo Sister KALPANA mara nyingi comments zake kama anatangaza biashara flani kinguvuuu!!!!
Naona hujasoma mwanzo wa hii ishu nitafute mahali nilipotoa comment yoyote mbaya kwenye thread yoyote ile. Bado huna hoja
Itaje hyo biashara Fulani ni gani mkuu ili nikuuzie na wewe
 
Ktk maisha yangu hakuna kinachonichukiza kama matusi
Halafu usiombee ukutane na ng'ombe iliyotoka malishoni! Yaani umechangia uzi fulani! Huku ukiwa huna hili wala lile, inatoka kusiko julikana na kuja kukutukania mama yako!

Aisee hakuna tusi ambalo sijawahi kulivumilia kama hili! Enzi zangu za ujana kuna mbwa wawili niliwahi kuwatandika ngumi za uso kwa sababu tu ya kunitukana hili tusi.
 
Back
Top Bottom