Simba SC imepangwa kundi gumu ila ratiba ya kundi itawabeba

Simba SC imepangwa kundi gumu ila ratiba ya kundi itawabeba

Mtamba wa Panya

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
764
Reaction score
1,892
Binafsi naona ratiba inaibeba Simba SC na kama watalitambua hilo, wanaweza kupenya kwenda robo fainali. Simba SC ataanza nyumbani na Saoura kabla ya kucheza mechi mbili mfululizo ugenini na AS Vita na Al Ahly.
Nimeshangaa sana kuona 'mashabiki' wengi wakikata tamaa baada ya makundi ya CAF Champions League kupangwa siku ya jana, wengi 'wakidai' kuwa tumepangwa na timu ngumu.
Sasa nikiyatazama hayo manne sioni kundi lolote rahisi kama watu wanavyodhani. Kumbukeni hii miamba 16 yote 'imepitia na kufaulu' mikikimikiki yote ya hatua ya mtoano mpaka kutinga makundi, tofauti ya hizi timu ni 'kujiamini tu' kunakotokana na uzoefu wa baadhi ya timu.
Strategy kuu zitumiwazo na vigogo wazoefu wa haya mashindano ni hii:
1. Kushinda mechi zote za nyumbani
2. Kutafuta suluhu ugenini ( au ukizubaa unapigwa kwako kwa counterattack)
Hivyo tuelewe kwamba Africa hakuna giants kama Real Madrid, Barcelona au Bayern Munchen ambao 'wanakupiga nje ndani' utake usitake.
Timu yeyote inaweza kufungwa ugenini na timu yeyote inaweza kushinda nyumbani (hata hao Al Ahly 'wanaowaogopa' baadhi ya watu, pia wamefungwa mechi ya mwisho na timu ya Ethiopia ugenini).
Sasa watu wanavyokata tamaa najiuliza walitegemewa kupangwa na timu gani wao wanaiona rahisi? Mamelodi Sundowns, Tp Mazembe, Asec, Wydad, Esperance au nani?? Au mnadhani Horoya AC ni kibonde? Hawa jamaa ni wababe sana hasa wakicheza nyumbani kwao na msimu ulioisha walifika hadi robo fainali ya CAF Champions League.
Timu pekee ninayoiona dhaifu kwenye makundi ni FC Platinum ya Zimbabwe, ila zingine zote ni wababe tusijidanganye.
Ni ujinga mwanaume umepambana na sasa umeshaingia kwenye makundi halafu unakata tamaa hata mechi moja hujacheza eti sababu kufungwa kwenye Azam Cup, haya ni mashindano tofauti yenye approach na psychology tofauti hata kwa wachezaji na viongozi. Inafungwa Real Madrid itakuwa Simba SC.!!
Hii tabia ya kukata tamaa inaonyesha ni aina gani ya watu tulionao kwenye jamii yetu, watu wavivu wanaotegemea ajira za serikali, yaani serikali isipotangaza ajira ni vilio kila Kona. Kwa nini wachaga wako tofauti na waafrika wengine? Jibu ni rahisi sana, hawakati tamaa kwenye maisha na wanapambana kweli kweli sawa na wahindi na waarabu wa Tanzania.
Hebu watanzania tuache hizi tabia maana ndio adui wetu mkubwa kwenye kila sekta na si michezoni peke yake.
 
true it can be done, our challenge is learning the enemy and combating to the best strategy, a best strategy will always contribute to the success and enhance determination to the fighting team. The African footfall is the same, strategies are different the west African country seems better on planning and executing their strategy of which if Simba needs to win should put time on coming with comprehensiveness plan within resources it has so as to make things happen.It can done!
 
Kwa hatua tuliyofika ni lazima tupambane na miamba (ndio level zetu) isitoshe hakuna timu dhaifu kwenye hiyo hatua na mwisho wa siku mpira hauna hatimiliki kama 2003 tuliwavua ubingwa Zamalek tukionekana wanyonge vipi leo tuogope miamba? Bila kutoboa mwamba hupati maji hata madini.
 
Timu 16 Bora za afrika utapangwa na nani mchovu... nafikiri haya ni maneno tu ila kwa uhalisia hakuna wa kubeza wote wamejipanga.
kuna timu ilipewa kundi lenye timu za ukanda huu wa afrika mashariki kwenye shirikisho na bado wakapwaya kabisa.
hakuna wa kubeza aisee.
 
Back
Top Bottom