Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Ukisoma gazeti la mwanaspoti la leo mama Karume anafafanua jinsi mgogoro ndani ya Yanga ulivyopelekea kujitenga kwa baadhi ya wanachama na kuanzisha Sunderland mwaka 1936. Kisha kuitwa Simba hapo baadaye. Kweli Yanga ni baba wa soka la Tanzania.
UPDATES:
Kwa habari zaidi soma;
http://www.mwanaspoti.co.tz/Soka/-/1799484/2144144/-/item/1/-/12344m8/-/index.html
UPDATES:
Sehemu ya hiyo habari hii hapa;
Aliyoyafanya Karume kwa Yanga
Mama Karume anasema: Sheikh Abeid AmaniKarume alikuwa mhamasishaji mkubwa wa kuanzishwa kwa klabu ya soka ambayo sasa ndiyo hii inayoitwa Young Africans Sports Club, yaani Yanga.
Baada ya kufanya kazi ya ubaharia iliyomwezesha kuzunguka karibu dunia nzima kwa miaka kadhaa akiwa kijana mdogo, Karume alipata uzoefu wa yaliyotokea kwenye nchi mbalimbali alizozunguka duniani na kugundua kwamba serikali za kikoloni zilipiga vita uanzishwaji wa vyama vya siasa vya wananchi wazawa, lakini zilikuwa hazipingi vyama vya kijamii kama klabu za michezo.
Baada ya kuufahamu ukweli huo, akiwa nyumbani Zanzibar, Karume alijiunga na wenzake na kuunda klabu ya soka iliyojulikana kwa jina la African Sports Club, mwenyewe akiwa mchezaji mahiri, humo humo kwenye mikutano ya kisoka ndimo yeye na Wazanzibari wenzake walikuwa wakijadili jinsi ya kujinasua kutoka kwenye utawala wa Kisultani uliokuwa ukilindwa na Waingereza.
Ni hayati Karume ndiye aliyehamasisha kuanzishwa kwa matawi ya hiyo African Sports ya Zanzibar na akafanikiwa kuanzishwa kwa tawi la timu hiyo jijini Dar es Salaam ambalo kwa sasa ndilo hii klabu kubwa sana ya Yanga na kule Tanga alifanikisha kuanzishwa kwa tawi jingine ambalo ni African Sports ya Tanga.
Kumbuka kuwa kwenye miaka hiyo ya nyuma, miji ya Dar es Salaam, Bagamoyo, Pangani na Tanga ilikuwa na ukaribu sana wa kiuhusiano na miji ya visiwa vya Unguja na Pemba. Kipindi kama cha Pasaka walikuwa wakitembeleana, klabu za kule zinakuja na wakati mwingine za huku zinaenda huko.
Baada ya kuanzishwa timu hizo tatu; Yanga ya sasa, African Sports ya Zanzibar na African Sports ya Tanga, zilitengeneza undugu wa damu kubwa mno. Zote tatu zilikuwa chimbuko la hayati Karume.
Lakini haikuchukua muda, mwaka 1936 Yanga ikakumbwa na wimbi kali sana la migogoro, baadhi ya watu wakajitenga kutoka Yanga na kwenda kuanzisha klabu yao ambayo iliitwa Sunderland ambayo ndiyo Simba.
Mwaka 1971, Karume aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi. Karume alitoa mchango wake wa fedha wa kufanikisha ujenzi wa jengo hilo, hapo hapo alitoa rai kwa klabu hiyo kuachana na jina la Sunderland Sports Club lililokuwa likitumiwa na klabu hiyo hadi wakati huo.
Hakuishia kuelekeza tu kwamba jina hilo lilikuwa haliakisi utamaduni wetu na lilikuwa mwendelezo wa mabaki ya ukoloni, bali pia alipendekeza jina linalotumika sasa na klabu hiyo nami nakumbuka waziwazi nilivyomsikia akisema kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam, alisema Achaneni na jina hilo la kikoloni la Sunderland kwani tuko Uingereza hapa? Mnaweza mkajiita Simba Mwekundu Sports Club, jina linaloeleweka na linaloendana na utamaduni wetu.
Kwa habari zaidi soma;
http://www.mwanaspoti.co.tz/Soka/-/1799484/2144144/-/item/1/-/12344m8/-/index.html