OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Ukiangalia uwezo wa timu zote zilizowahi kuitoa Simba Sc robo fainali,ni timu zenye kasi sana. Orlando Pirates na Kaizer Chiefs. Angalia pia timu zinazopenya nusu fainali,hakuna timu inayocheza slomo.
Usajili uliofanywa na Simba kwa Augustine Okra na Phiri ikiwemo anayetajwa kusajiliwa Okwa ni machine zinazocheza kasi sana. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba Simba hatukurupuki tunasajili kulingana na malengo ya timu.
Kinachobaki hapa ni kumaliza sajili ya Cesar Manzoki ambaye ni striker anayelijua goli akimalizia kazi nzuri za Phiri, Okwa na Okra. Bila kusahau beki matata la kuanzisha mashambulizi Qattara au Herve.
Strategic Plan ya Simba ni kuwa timu kubwa Africa kisoka na kirasiliamali