Simba SC kwa aibu kubwa ninayoiona inakuja na kwa upuuzi wa Ndola jana, tuwape Yanga SC nafasi yetu AFL ili wakaliheshimishe Taifa

Ni mwana Simba SC Mpumbavu ( Fool ) tu ambaye kwa Mpira mkubwa Unaochezwa sasa na Yanga SC ndiyo atakataa na atabisha kuwa Yanga SC hawaendi kuwa Mabingwa tena kwa Msimu huu na kwa mara ya Tatu mfululizo.
Kwa Timu ile ya Power Dynamos FC ni ya kutoa Sare nayo Kweli Mkuu? Tusifiche ukweli kuwa Simba SC bado tunajitafuta na tuna Kikosi dhaifu Kimashindano.
Kuna ukweli fulani hapo.
 
Simba sjui kwann hawakusajili mbadala wa kapombe na tshabalala, mana Kwa jicho la kishabiki tu msimu ulopita ilifaa kabisa kusajili fundi haswa atakae fanya KAZI kuwapa Chachu Hawa jamaa.

Malogne ni mzuri taabu anafanya KAZI kubwa mno kiasi anakosa umakini na kuonekana kua na makosa flan yanayoweza garimu mchezo kiujumla. Apunguziwe majukum.

Hapa kwenye kiungo sasa ndo wavivu kupindukia namuona Mzamiru akijaribu kutuliza mshambulizi japo anagame zake.
 
Simba kafanya haya uyaonayo leo kabla ya yanga kujulikana, Simba ameliheshimisha taifa kwa style hiihii labda kama ulkua bado hujazaliwa
 
Simba wana wachezaji wazuri kuliko yanga walichotuzidi yanga wachezaji wao wana fighting sprit. Wachezaji wa Simba hawajitumi wana usupastaa mwingi wengi hawana ndoto za kuchezea timu kubwa ndoto zoa zimefika Mwisho.
Hebu tuanze kuwalinganisha mchezaji mmoja mmoja tuone kama wachezaji wetu kama hata 3 tunaingiza first eleven timu zikiunganishwa.

Tuacheni mahaba jamani.
 
Simba wana wachezaji wazuri kuliko yanga walichotuzidi yanga wachezaji wao wana fighting sprit. Wachezaji wa Simba hawajitumi wana usupastaa mwingi wengi hawana ndoto za kuchezea timu kubwa ndoto zoa zimefika Mwisho.
Wangekuwa wanajituma Simba Jana angetoka na goli sio chini ya nne, halafu kocha hakuwa na sababu ya kumwacha kibu aendelee toka pale alipopiga mpira juu mawinguni , kocha alikuwa na sababu gani kuchelewesha Sub?
 
Kaka mkubwa! Hakika umechafukwa hata hivyo hongera kwa ushindi wa jana. Wenzako tumeshinda ugenini kotekote.
 
Ufunguzi wa hiyo Ligi ya Uteuzi utafanyika Dar es salaam tarehe 20 October kwa Mkapa ngoja tusubiri hao National ingawaje na wao hawana Timu pia niliona wakikimbizwa mno na Alger juzi..daah sema Simba upangaji wa Timu unawasumbua mno na yule Boko kama mnampenda mpeni asaidiane na Kocha benchi la ufundi kuliko kutembea tuu Uwanjani..
 
Yanga bado hajacheza na timu bora .


Mwaka jana kwenye looser cup alibahatika vibonde mwaka huu tena kapata vibonde.


Tuvute subira tuone makundi kama atapata upepo wa vibonde au vipi.


Napenda yanga apate kundi kama hili tuone huo mpira anaosema anakikosi imara kama atatoboa.


 

Una machungu, umewahi hata kuchangia maendeleo ya Simba? Una kadi ya uanachama au unabwata tu hapa? Kaa kimya kima wewe!
 
Mkuu, Binafsi naona mechi ya jana kosa ni kocha alikosea kupanga kikosi 1st half. Alirekebisha hili kosa 2nd half. Goli la pili ni kosa la kipa. Simba ilikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda. Matokeo si mabaya. Nafasi ya kupita ni kubwa.
Kocha ambaye umeshakaa na timu muda huwezi kushindwa kujua 11 eleven yako ya ushindi, iligoma ndipo ingiza super subs..
 
Lakini walikandwa 2-0 na Simba kwenye ngao ya hisani.

Sisi hatuna kitu kinaitwa ngao ya hisani, hiyo ilishabakia historia, dunia nzima ngao ni ya jamii hakuna kitu siku hizi kinaitwa ngao ya hisani!
 
Bado tunacheza vizuri tusikate tamaa vijana bado wanao muda wa kujipanga kwa ajili ya mechi ijayo
Tuwaamini
Sare ya 2 kwa 2 haina baya lolote kwetu
Naamini ushindi upo

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Timu ile ya Power Dynamos FC ni ya kutoa Sare nayo Kweli Mkuu? Tusifiche ukweli kuwa Simba SC bado tunajitafuta na tuna Kikosi dhaifu Kimashindano.
Umeongea point, ukweli Simba SC imecheza mpira dhaifu hakuna muunganiko wa kitimu. Haiwezekani hadi leo hii timu haijaimarika bado inajitafuta na muda unaenda. Kuna wachezaji wazuri tu waliosajiliwa hatujawahi kuwaona wakipewa nafasi ys kucheza. Sijui kwa nini Viongozi na Menejimenti hawalioni hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…