Huyo simba haoneshi taswira ya kuunguruma bali anapiga miayo, pili kauli mbiu ya simba haipo,, tatu kwenye jezi hivi niwaulize hawana designer ? Mbona kila jezi mpya itolewayo kila msimu afadhali ya ile msimu uliopita, hii ina maana gani lakini ? Kiufupi wamefeli Mno
Sasa hzi ni jezi gani!??
Jezi kama za Vingunguti Fc!??
Hatuna jinsi tutazivaa tu hivyo hivyo ndio timu yetu
Bila shaka ni Utopoloacha kufananisha VINGUNGUTI FC na vitu vya hovyo hovyo!
Logo ya Liverpool hamna kauli mbiu? Embu itazame vizuri.Kwenye logo za Man U,Arsenal,Liverpool kuna kauli mbiu gani? Au unataka logo yenye Mabondia,Wacheza Rede,na Kauli mbiu hapohapo wakati sote twajua ni Logo ya Club ya mpira wa miguu tu!
Logo ya Liverpool hamna kauli mbiu? Embu itazame vizuri. View attachment 1537322
Lengo langu ilikuwa ni kukuonesha ya kwamba kwa upande wa Liverpool umeongopa au hulikuwa haujui au labda ulijisahau kuwa Liverpool wameweka kauli mbiu kwenye nembo yao.Leta na na logo ya Man U,Arsenal,Chelsea na Tottenham hapa!
Lengo langu ilikuwa ni kukuonesha ya kwamba kwa upande wa Liverpool umeongopa au hulikuwa haujui au labda ulijisahau kuwa Liverpool wameweka kauli mbiu kwenye nembo yao.
Nachojua mimi kila timu ina maamuzi yao ya kuweka logo wanavyotaka wenyewe iwavyo. Iwe na kauli mbiu au isiwe na kauli mbiu ni maamuzi tu. Au unataka kusema Liverpool walioweka kauli mbiu wamekosea?Na point ya msingi hapa ni kwamba kati ya Team 5 nilizozitaja hapo juu,4 logo zao hazina kauli mbiu na hiyo moja ndiyo inayo! Maana yake 80% ya logo za Team hazina kauli mbiu,so Simba wako sahihi zaidi na logo yao mpya! Hoja ya kwa nini nembo mpya haina kauli mbiu so hoja tena!
Jezi imetulia sana hii.Simba tunajezi mbovu sana.
Huu ndiyo umbumbumbu aliousema Rage
Huu ndiyo umbumbumbu aliousema Rage
Kwenye jezi simba tunapuyanga sana