kelele kwenye mpira wa miguu ni jambo la kawaida, Tambo,vijembe na misemo ya kejeri ni vitu vya kawaida kwa washabiki wa timu hasimu/pinzani au Watani wa Jadi.hyo ipo hivyo duniani kote.Sasa sijaelewa hoja yako hapa ni ipi? kwamba ulitaka washabiki wa Simba wasishangilie ushindi wao wa bao 7-0?,pia ulitaka washabiki wa Simba wasitambe kwamba watachukua ubingwa?,pia ulitaka washabiki wa simba wasiicheke Yanga kwa kutoka droo na lipuli?.Kama kweli hayo ndo ulikuwa unayataka basi inawezekana umeanza kushabikia Yanga na kupenda mpira kwa ujumla kipindi hiki cha Magufuli. Tambo kati ya washabiki wa Simba na Yanga zilikuwepo toka kipindi cha Nyerere na zitaendelea kuwepo siku zote,kama wewe zinakukwaza basi ujue tatizo lipo kwako wewe na njia pekee ya kukupa amani ni kuachana kabisa na Ushabiki wa mpira wa miguu,tuachie sisi tunafurahia hzo kelele za washabiki tuendelee kuenjoy.