Simba SC: Mimi siyo Muumini wa Kuaminishwa 'Kipropaganda' na Matokeo ya 'Mechi Mazoezi' huko Kambini Misri

Simba SC: Mimi siyo Muumini wa Kuaminishwa 'Kipropaganda' na Matokeo ya 'Mechi Mazoezi' huko Kambini Misri

Mi mwenyewe sijaelewa uyu kocha anatumia stahili gani, kocha mgeni, baadhi ya wachezaji ni wageni, sasa ameingia kambini siku 3 siku ya 4 kaomba mechi ya majaribio? Hii kiufundi sijaielewa, mi ninachojua kocha mpya anahitaji si chini ya wiki 6 kuingiza ufundi wake na mifumo yake mazoezini ikiwemo kuwafahamu wachezaji wake ipasavyo, sasa uyu bwana kaingia na gia kubwa mambo ni chap chap sijui kama na wachezaji wanashika icho anachofundisha
Big Results Now BRN

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hapa lazima ufundishwe tu, hata kama ukiwa certified popoma, PhD!.

Mechi ya kirafiki kocha anaweza kuitisha hata baada ya siku moja, kwa sababu zifuatazo;

1. Kocha akiwa mgeni.

2. Kujua uwezo wa wachezaji wake [kimbinu, kimwili, na kiakili] na mapungufu yao, ili kocha ajue wapi pa kuanzia kwenye mazoezi yake.

3. Mechi za kirafiki zinamjengea mchezaji hali ya kujiamini, na kumpa nafasi mchezaji husika kuonesha uwezo wake mbele ya kocha mpya.

4. Kocha anaanza kupata picha ya mfumo atakaotumia kulingana na strength atakazoziona kwa wachezaji wake kwenye mechi za kirafiki.

Popoma kariri hizo kwanza!.
Kwa sehemu nimemuelewa mleta mada.

Kocha alipaswa akae na timu ili kwanza kabisa kuzoea mazingira ya kazi, pili alipaswa akitambue kikosi chake vyema, hapa lazima akae kambini ata kwa wiki mbili na ili kupata muda zaidi ya kutambua weakness na strenght za squad yake.

Baada ya kutambua weakness na strenght za kikosi chake, anakuja kuanza kutengeneza yale madhaifu ili aendane na ile plan ambayo yeye amekuja nayo, yaani mapendekezo ya mifumo ya uchezaji alopewa na muajiri wake au ile ambayo yeye ameiona ni vyema kutokana na profession yake.

Sasa huwezi kuanza Game ya kirafiki bila wewe mwenyewe walau kujenga taswira ya timu unayoitaka. Sasa utajuaje mifumo uliyoingiza mpaka muda huo imeanza kufanikiwa kwa namna gan? Kipi utoe na kipi uingize?

Kwa namna hii, Ngao ya Jamii itakuja kupigiwa kipindi ambacho bado Kocha hajakiandaa kikosi chake vyema.
 
Kwa akili ya kawaida kocha katrain siku 3 na ya 4 kaomba mechi ya majaribio, kocha mpya, usajili kasajili wapya, kiufundi iyo kitu inaitwaje?
Wanamponda bure mleta mada ila ukitazama hili jambo kwenye jicho la mpira bila kuweka mapenzi ya kipumbavu, mleta mada yupo sahihi.
 
Mi mwenyewe sijaelewa uyu kocha anatumia stahili gani, kocha mgeni, baadhi ya wachezaji ni wageni, sasa ameingia kambini siku 3 siku ya 4 kaomba mechi ya majaribio? Hii kiufundi sijaielewa, mi ninachojua kocha mpya anahitaji si chini ya wiki 6 kuingiza ufundi wake na mifumo yake mazoezini ikiwemo kuwafahamu wachezaji wake ipasavyo, sasa uyu bwana kaingia na gia kubwa mambo ni chap chap sijui kama na wachezaji wanashika icho anachofundisha
Nahisi kocha yupo pale kwa niaba ya watu fulani, kwahiyo anafanya yale anayopangiwa, lakini ninaamini kabisa hata yeye hakuwa tayari kucheza hii mechi.
 
Mbona rahisi tu, huko ulaya ligi pendwa na ngumu na iliyojaa makocha vichwa. Timu inatimua kocha less than a week kuna mechi ya ligi ya mashindano kocha mpya anakuja anafanya yake.

Kulikoni kwa simba iwe Blah.! Blah.! Blah.!? Na simba ni mechi tu ya kirafiki.
Anyway Utofauti Ndio Utamu.
 
Huyu sasa ndiyo GENTAMYCINE, the Genius from SAUT ninayemfahamu! Sijui ni kwa nini hawakupi nafasi ya CEO pale klabuni!

Hakika simba ingekuwa kama Real Madrid ndani miaka 5 tu ya uongozi wako. Yaani mpaka wakati huu, nahisi IQ yako itakuwa ni mara dufu ukilinganisha na ile ya Ismail Aden Rage!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kisa amekufurahishaa ulichotaka kusikia??
Bas hapo uko buheriiii mwenyewe.

Byuti byuti bhanaa. Uwiiiih
 
Jamaa kaongea uharo alafu kapotea. Hemu tuambie wachezaji wapya wangapi wamrcheza kwenye hiyo mechi
 
Dah kukosoa hua ni kazi rahis kwel, mtoa anadhan mwalimu anaanza na mfumo kabla ya kujua wachezaji alionao, Ila kwa Hali halisi wachezaji ndio wanamuonesha mwalimu atumie mfumo gan Ila pili coach ana kazi ya kupunguza wachezaji wawili ama watatu, sio kazi rahisi hata kidogo. Na wachezaji wanapojua wanatafuta kubakia kikosini hujituma Sana mazoezini.

Heb mashabiki tubakie na jukumu letu la kushangilia, coaching ni proffesional iheshimiwe, kama unadhan ni rahis kasome uone Kama utapata timu hata ya daraja la tatu.
 
Wanamponda bure mleta mada ila ukitazama hili jambo kwenye jicho la mpira bila kuweka mapenzi ya kipumbavu, mleta mada yupo sahihi.
Siku zote huwa naeleweka vyema na haraka na Watu Werevu ( Intelligent ) kama Wewe, ila Wapumbavu na Waswahili huwa hawanielewi na badala wanaishia Kunichukia tu huku Mimi nikiendelea Kuwadharau zaidi.
 
Back
Top Bottom