Mkuu kurenew mkataba hakuna Athari katika mkataba wa awali ispokuwa mtakubaliana tu terms mpya kwenye mkataba mpya unless otherwise uamue kuvunja mkataba ili uangalie maslahi kwingine, hivo mnaweza kurenew mkataba mpya ukiwa bado unautumikia mkataba wa zamani
Mkataba wa man u na Chevrolet's ulisainiwa msimu wa mwaka 2014/2015 na mwisho wa mkataba ni msimu wa 2020/2021 ila kutokana na Mambo ya COVID Man u wakakosa sponsor mpya ikabidi wa extend tena mkataba na Chevrolet's
Kwenye hii mikataba waga wanapiga hesabu za kupanda thamani club ndomana waga kila mwaka inapanda, kwahiyo ukiangalia rates ya ongezeko la hela Kwa Simba hiyo ndio hesabu ya thamani yake Kwa kila mwaka
Arsenal na Fly Emirates waliingia mkataba wa kukaa mbele ya jezi mwaka 2006 hadi mwaka 2018, na waka extend tena mpaka 2024, ndio mkataba utaisha, kuna PSV Eindhoven walisaini mkataba wa zaidi ya miaka 20 na kampuni ya Philips
Kwahiyo ukiangalia Kwa man u walisaini mktaba wa miaka 6, na arsenal walisaini mkataba wa miaka 12, kwahiyo hao wote hawajui kama thamani ya club zao zinapanda ila wewe ndio unajua sana
Simba inaweza ikafeli kwenye mafanikio ya uwanjani ila sio kwenye biashara mkuu, Yule Barbara Yuko vizuri sana kwenye issue za biashara na ndio yeye anaiongeza thamani ligi ya NBC kutokana na misimamo yake kwenye mikataba
Barbara Tangu awe CEO wa Simba kaingia mikataba ya kikubwa sana, kwenye biashara anajua vizuri dunia inaenda wapi maana ndio field yake ilipo hivo nategemea ataendelea kuleta wawekezaji wengi na wenye tija
Mkataba na Mbet unahusu team moja tu ya senior, kwahiyo kuna room ya kuona wawekezaji wengine kwenye Simba Queens na ata under 20 pia, ndio ujue ni namna gani huyu dada ye anawaza kupandisha thamani ya club yake