Simba SC Msiogope Kuwaiga Amazulu FC

Simba SC Msiogope Kuwaiga Amazulu FC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Leo asubuhi nimepata nafasi ya kuwa pamoja na mmoja wa kuongozi wenu. Yaani ni miongoni mwa wanakamati wa ile Bodi yenu.

Nilikuwa napiga nae stori mbili tatu viwanja fulani hivi hapa jijini Dar. (si mnajua mambo ya wikiend).

Katika stori akatanabaisha wazi kuwa viongozi wa klabu yenu wamegawanyika katika pande kuu mbili.

Moja:
Inataka kikosi kizima kifumuliwe, yaani waachwe wachezaji wengi kwa wakati mmoja. Wachezaji ambao wana above 33yrs plus local players ambao hawajafanikiwa kuonyesha ushindani.

Mbili:

Huu upande ni ule una idadi kubwa ya viongozi wenye kujaa hofu kwamba kikosi kisifumuliwe bali wapatikane wachezaji wagharama kubwa kama 3 tu ili waone kama watasaidia mtumbwi usizame msimu ujao.

Kundi la kwanza linapendekeza kuondolewa wachezaji wengi kwa mkupuo na kununua wachezaji wengi kwa bei nafuu.

Hilo kundi la pili linahofu kubwa sana kuhusu kuwapo wa wachezaji wengi wapya ambao wataleta changamoto ya kupatikana chemistry kwenye kikosi.

Na ndio sababu ilapelekea hata dili la Adebayor kuingiliwa kati la Berkane huku wao wakibaki wanajibizana.


Kiongozi huyo ikafika hatua akaanza kulalamika kuwa mgawanyiko huo ndio umewarahisishia hata Yanga SC kukamilisha mkataba wa awali na Azizi Ki.

Ushauri wangu ni kwamba msiogope kuondoa wazee hapo klabuni kwenu kwa hofu ya wachezaji wapya kukosa connection mapema.

Bali fanyeni uamuzi wa kweli maana next season Yanga SC watakuja kuwakwaruza panye kidonda..

View attachment 2257546
 
Aziz Kii amesajiliwa Red Bull Berkane huyo waliomsajiri Uto ni Aziza Kaisi kiungo wa Timu ya taifa ya wanawake Sudan kusini
FB_IMG_16549600626108034.jpg
 
Aziz Kii amesajiliwa Red Bull Berkane huyo waliomsajiri Uto ni Aziza Kaisi kiungo wa Timu ya taifa ya wanawake Sudan kusini

Alicho wafanyieni Berkane mpaka muda huu hamuamini macho yenu...

[emoji23][emoji23]
 
Hilo kundi la pili ndio wapo sahihi. Nitaelezea huo usahihi.

1. Tatizo la simba kwa sasa si wachezaji ni benchi la ufundi. Hakuna timu duniani wachezaji wakashuka viwango kwa wakati mmoja. Kagere,Mugalu na Bocco walimaliza kama wafungaji bora lakini msimu huu hata goli kumi hawajafika. Lwanga,Bwalya na Chama je nao ni wabovu? Wachezaji wapewe muda.

2. Ukipunguza wachezaji wengi kwa wakati mmoja unaua roho ya timu(chemistry) na naona wanaosupport hii kitu ni wazee wa "kamisheni" hamna namna zaidi ya hapo.

Simba itulize kichwa chini waache kufanya mambo kwa emotions tutaanguka zaidi ya huu msimu.
 
Aziz Kii amesajiliwa Red Bull Berkane huyo waliomsajiri Uto ni Aziza Kaisi kiungo wa Timu ya taifa ya wanawake Sudan kusini
Unaswali jingine?
 

Attachments

  • FB_IMG_16549606003339059.jpg
    FB_IMG_16549606003339059.jpg
    54.7 KB · Views: 7
  • FB_IMG_16549605919196440.jpg
    FB_IMG_16549605919196440.jpg
    37 KB · Views: 7
  • FB_IMG_16549606117180508.jpg
    FB_IMG_16549606117180508.jpg
    37 KB · Views: 9
Back
Top Bottom