Simba SC Msiogope Kuwaiga Amazulu FC

Simba SC Msiogope Kuwaiga Amazulu FC

Hilo kundi la pili ndio wapo sahihi. Nitaelezea huo usahihi.

1. Tatizo la simba kwa sasa si wachezaji ni benchi la ufundi. Hakuna timu duniani wachezaji wakashuka viwango kwa wakati mmoja. Kagere,Mugalu na Bocco walimaliza kama wafungaji bora lakini msimu huu hata goli kumi hawajafika. Lwanga,Bwalya na Chama je nao ni wabovu? Wachezaji wapewe muda.

2. Ukipunguza wachezaji wengi kwa wakati mmoja unaua roho ya timu(chemistry) na naona wanaosupport hii kitu ni wazee wa "kamisheni" hamna namna zaidi ya hapo.

Simba itulize kichwa chini waache kufanya mambo kwa emotions tutaanguka zaidi ya huu msimu.
Mafanikio hayaji siku moja,,kwenye soka inahitaji uwekeze pesa then uwe mvumilivu ,so kwa kesi ya simba swala la kuacha wachezaji ni sahihi kwao maana wengi wao wameshatumika zaid ya misimu mitatu na consistency yao imeshuka mfn mugalu,kagere,bocco,wawa,thadeo,gadiel hawa wote wanastahili kuachwa then timu ijengwe upya kwa wachezaji wapya but simba hofu yao ni kuwa ni kukosa chemistry msimu ujao n kwel kikosi kitahitaji mudaa ili tu wafikie lengo lao la kubwa la kuja kubeba kombe la africa uvumilivu unahitajika kwa sasa katika timu
 
Kiongozi huyo ikafika hatua akaanza kulalamika kuwa mgawanyiko huo ndio umewarahisishia hata Yanga SC kukamilisha mkataba wa awali na Azizi Ki.
Nadhani lengo lilikuwa kuongelea Ki. Umezunguuka, basi sawa taarifa wamezipata.
 
Mm niliwaambia Side hana hela ila yeye ni dalali tu anatumiwa na watu kuipora Yanga na hili wamefanikishwa na walitumia excessive nguvu kuchukua makombe ili watimize adhima yao ovu, masikini yanga ileee inaangamia
Kama Yanga inaangamia basi Simba ndio itafutika kabsaaaa kwa mwendo ule wa mudi
 
Leo asubuhi nimepata nafasi ya kuwa pamoja na mmoja wa kuongozi wenu. Yaani ni miongoni mwa wanakamati wa ile Bodi yenu.

Nilikuwa napiga nae stori mbili tatu viwanja fulani hivi hapa jijini Dar. (si mnajua mambo ya wikiend).

Katika stori akatanabaisha wazi kuwa viongozi wa klabu yenu wamegawanyika katika pande kuu mbili.

Moja:
Inataka kikosi kizima kifumuliwe, yaani waachwe wachezaji wengi kwa wakati mmoja. Wachezaji ambao wana above 33yrs plus local players ambao hawajafanikiwa kuonyesha ushindani.

Mbili:

Huu upande ni ule una idadi kubwa ya viongozi wenye kujaa hofu kwamba kikosi kisifumuliwe bali wapatikane wachezaji wagharama kubwa kama 3 tu ili waone kama watasaidia mtumbwi usizame msimu ujao.

Kundi la kwanza linapendekeza kuondolewa wachezaji wengi kwa mkupuo na kununua wachezaji wengi kwa bei nafuu.

Hilo kundi la pili linahofu kubwa sana kuhusu kuwapo wa wachezaji wengi wapya ambao wataleta changamoto ya kupatikana chemistry kwenye kikosi.

Na ndio sababu ilapelekea hata dili la Adebayor kuingiliwa kati la Berkane huku wao wakibaki wanajibizana.


Kiongozi huyo ikafika hatua akaanza kulalamika kuwa mgawanyiko huo ndio umewarahisishia hata Yanga SC kukamilisha mkataba wa awali na Azizi Ki.

Ushauri wangu ni kwamba msiogope kuondoa wazee hapo klabuni kwenu kwa hofu ya wachezaji wapya kukosa connection mapema.

Bali fanyeni uamuzi wa kweli maana next season Yanga SC watakuja kuwakwaruza panye kidonda..

View attachment 2257546
.
FB_IMG_1611660294488.jpg
 
Back
Top Bottom