Simba SC mtaendelea kupata mnachostahili mpaka mkubali timu yenu kwa sasa ni maji maji iliyochangamka

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Nafikiri tutaendelea kuelewana mdogo mdogo kwa wale mashabiki oya oya wa simba ambao ni mbumbumbu wa kuiangalia timu yao kiufundi Ina matatizo gani, sasa aya yanayotokea sio kwa bahati mbaya bali ni uwezo wa timu ya simba uko chini sana, na Kama awatashtuka kurekebisha mambo na kuendelea kujifanya wako vizuri uwanjani wataendelea kupokea matokeo Kama aya.

Sijaona clear chance ata moja ambayo simba wameitengeneza kufunga goli, achana na mipira ya kibu Denis ambayo uwezi kusema ni clear chance kwakuwa alikuwa amezongwa na mabeki.

Simba awa awa walikuwa wanaizodoa yanga kwamba uwanja wa taifa yanga inafunga kagoli kamoja kwanini, lakini wao wamepata goli la penalti na Leo wameshindwa kupata ata ilo la penalti licha ya kucheza na timu pungufu mda mrefu, Mkubali mkatae simba iko gonjwa
 
Tatizo ni viongozi kuingilia benchi la ufundi.. Wanajua wazi wachezaji wengi wakigeni wa mwaka huu "wametupiga"" ila wanalazimisha wacheze.

Asante Mungu leo kawaumbua kwa kuumia Kanoute,Mmeona mambo waliyoyafanya Muhilu,Mkude na Morrison. Kuanzia sasa kikosii tunapanga sisi wanachama mpaka mtakapopata mwalimu anaeleweka.

Mechi ijayo kikosi ni ..Manula, Kapombe,Mohamed,Wawa, Onyango,Mudhamiru,Muhilu,Mkude,Kagere,Bwalya na Morrison
 
Nashindwa kuelewa... Kagera Sugar, Dodoma Jiji, Mtibwa Sugar, Polisi Tanzania, Ruvu Shooting, Biashara wanatengeneza nafasi wakiwa na wachezaji wa kawaida ila kwa Simba japo wana mapro lakini zile chance za kufunga hazionekani....

Tatizo mfumo, uchovu, kuridhika na mafanikio, uwezo mdogo au viwango vimeshuka.!???
 
Mtoe Wawa hapo... Kuna mwamba 'Stopper' Kennedy Juma......
 

Mchanganyiko wa yote uliyosema
 
Kwa hiyo Coastal sio tawi la Simba tena?
Litaendelea kuwa tawi na wao wameona kinachobebwa akibebeki wakaamua kukomaa nao tu, mchezaji Kama anawekewa mpira afunge anashindwa wangefanyaje sasa
yanga wamepenyeza mpunga si unaona hata jezi ya coastal union kuna tangazo la GSM
Mtaendelea kuiimba yanga mpaka midomo yenu itapinda kudadadeki, sasa hivi ata yanga wakijamba mtasema aliyejamba kahongwa na gsm
 
Utulivu haupo kabisa yaani kiufupi saikolojia ya wachezaji tayari imeshaharibika haswaaa,presha ya kutaka matokeo kwa Hali na Mali imewajaa wachezaji na benchi la ufundi lote kupitia viongozi wa klabu,ni kipindi kigumu Sana kwa wachezaji,benchi la ufundi la Sasa walifanye kulibadilisha haraka Sanaa naona kabisa benchi halina ile roho ya uongozi au mamlaka.

Cha msingi na Cha umuhimu ni kwamba watu wawe na subira tu,Simba ya misimu iliyopita haiwezi kujirudia kwa asilimia 100 kwa msimu huu, yaani watu wanampa mzigo mkubwa Sana Bwalya as if ndo mchezaji peke yake,amezungukwa na wachezaji wanaohitaji muda Sana ili waweze kucheza vizuri,kijana sadio kanoute bado bado Sana pasi anazopiga siyo zile watu walizotegemea yaani bado Hana accuracy nzuri ya upigaji pasi Hadi Sasa hivi.

Mbavu ya kulia tayari Sasa hivi kiza kimeingia kwenye ile mbavu siyo Tena yule shomari wa misimu iliyopita....timu ya Simba shida kubwa Sasa hivi ni kushughulikia saikolojia ya wachezaji na mbinu za kiufundi(Benchi kuu la ufundi) nafikiri haya mawili yanaweza kusaidia Sana licha ya changamoto nyingi za wachezaji husika wa Sasa hivi,tusilazimishe Simba hii icheze Kama ya misimu mitatu iliyopita...
 
Kwa Mkapa gemu ya Simba 0 vs coastal Union 0 imemalizika ila biriani sikuliona wewe je? Nimeona tu nyoni Leo ndo alikuwa mkuu wa benchi la ufundi.
 
yanga wamepenyeza mpunga si unaona hata jezi ya coastal union kuna tangazo la GSM
Na mechi ijayo tunawahonga wachezaji wenu wote kudadek!! Yaani mpaka wale wa akiba.

Vibabu vyenu vyote mfano Onyango, Kagere,Nyoni, nk tunavianzishia bima ya afya na kuvilipa kabisa mafao yao.
 
Utulivu haupo kabisa yaani kiufupi saikolojia ya wachezaji tayari imeshaharibika haswaaa,presha ya kutaka matokeo kwa Hali na Mali imewajaa wachezaji na benchi la ufundi lote kupitia viongozi wa klabu,ni kipindi kigumu ...
Umeongea kiufundi sana kuliko hao wanaolalamika,suala la benchi la ufundi kukosa mamlaka nimeliona kocha hitimana ni kama vile hawezi kulitawala benchi lenye waswahili matola na manager Rweyemamu,inaitajika kocha atulize benchi lake awe na mbinu zake na azisimamie lakini akisikiliza kelele za wakina matola hakuna kitu atafanya
 
Matola ni kocha msaidi, kuna ubaya gani kumsikiliza? Kama mnaona Matola hana wadhifa wa kusikilizwa basi mumfukuze kisha mlete kocha mwingine msaidizi atakayestaili kusikilizana na kocha mkuu. Naona timu inawayumbisha akili mnaongea sababu zingine kama sio watu wa mpira vile
 
Ubongo wako haujajaa ndio maana umekurupuka,nimeandika kuhusu kocha mkuu kulitawala benchi la ufundi na mbinu na mipango yake ndio iwe msingi wa benchi na sio kufika na kuanza kuelekezwa na kocha msaidizi,uwe unatafakali kwanza kabla ya kujibu,au wewe ni mke wa matola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…