Simba Sc na Morison

Simba Sc na Morison

Kwanza awali ya yote niipongeze klabu cha Yanga kwa kutwaa ubingwa Jana.

Moja kwa moja kwenye mada.Niseme tu wazi kwamba huyu Morison inatakiwa apewe ushauri abadilike.Haiwezekani anapewa pesa kuliko mchezaji yeyote halafu hana msaada wowote kwa timu.Imagine wachezaji key players wengi hawapo lakini wewe unayepata hela zote hizo unakaa benchi dk zote 90.

Unaweza kusema umlaumu kocha kutomuingiza lakini ni ukweli usioweza kupigwa kwamba kocha anaona hatakua na msaada wowote ko ni bora yule aliyechoka uwanjani aendelee tu.Unaona kabisa Jana Kahata kachoka na kazidiwa ila nani aingiee!!

Wito kwa viongozi wa Simba ,huyu bwana apewe ushauri aache utoto.Mashabiki hatutaki mbwembwe na utoto utoto kabisa.

Uongozi pia umpeleke mtu kama Ajibu timu nyingine akapevuke.Hii Simba ni ya kimataifa.Si ya kuja kufanya mzaha.Chonde chonde
USILOLIJUA! USIKU WA KIZA !!!
 
Vp tena mnaanza kulia lia,mwamedi si alisema ameongea naye atabadirika......?? Tabia ya mtu ningumu kubadirika......mlidhani mnaikomoa The Citizens,kumbe mnajitia dole wenyewe....saizi mpelekeni tu milembe
 
USILOLIJUA! USIKU WA KIZA !!!
Hakuna cha kiza wala nn...Timu ya Simba haihitaji wachezaji wasanii na wavivu...Ajibu kwa mkopo ,huyu Morison waongee naye.Asipobadilika naye apelekwe kwny timu ndogo akakue.Simba instakiwa kua na wachezaji wenye spirit ya kupambana kama kwa wachezaji wengi wa Yanga.La sivyo tuna hatihati kubwa ya kuchukua ubingwa msimu huu
 
WAMEINGIA CHA IKE WAAAAH! CHAKIKEEEE....... Morrison ana Busha. Habari take KWA SOKA LA bongo kwisha.
 
Baada ya mechi akaenda kukaa sehemu waliyopo wachezaji wa Yanga. Huyu jamaa atakuwa anashida kichwani.
Kumbe na wewe uliona ,huyu jamaa anadhani anakomoa watu ,alikuwa anapasha baada ya kuona hajaingizwa ndo akaenda kukaa huko kwa wachezaji wa yanga ,nasikia majeraha ni uwongo ,ukweli ni kwamba Simba walikasirishwa na hicho kitendo chake
 
Kumbe na wewe uliona ,huyu jamaa anadhani anakomoa watu ,alikuwa anapasha baada ya kuona hajaingizwa ndo akaenda kukaa huko kwa wachezaji wa yanga ,nasikia majeraha ni uwongo ,ukweli ni kwamba Simba walikasirishwa na hicho kitendo chake
Uzuri hata yeye mwenyewe ashagundua fika kwambasi tegemezi hata kidogo ndani ya Simba Sc.Asiposhtuka mapema ,basi atafungashiwa virago muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom