Akthoo
JF-Expert Member
- Nov 5, 2007
- 1,001
- 1,021
USILOLIJUA! USIKU WA KIZA !!!Kwanza awali ya yote niipongeze klabu cha Yanga kwa kutwaa ubingwa Jana.
Moja kwa moja kwenye mada.Niseme tu wazi kwamba huyu Morison inatakiwa apewe ushauri abadilike.Haiwezekani anapewa pesa kuliko mchezaji yeyote halafu hana msaada wowote kwa timu.Imagine wachezaji key players wengi hawapo lakini wewe unayepata hela zote hizo unakaa benchi dk zote 90.
Unaweza kusema umlaumu kocha kutomuingiza lakini ni ukweli usioweza kupigwa kwamba kocha anaona hatakua na msaada wowote ko ni bora yule aliyechoka uwanjani aendelee tu.Unaona kabisa Jana Kahata kachoka na kazidiwa ila nani aingiee!!
Wito kwa viongozi wa Simba ,huyu bwana apewe ushauri aache utoto.Mashabiki hatutaki mbwembwe na utoto utoto kabisa.
Uongozi pia umpeleke mtu kama Ajibu timu nyingine akapevuke.Hii Simba ni ya kimataifa.Si ya kuja kufanya mzaha.Chonde chonde