Simba Sc na Morison

Simba Sc na Morison

endesha

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2015
Posts
1,297
Reaction score
1,877
Kwanza awali ya yote niipongeze klabu cha Yanga kwa kutwaa ubingwa Jana.

Moja kwa moja kwenye mada. Niseme tu wazi kwamba huyu Morison inatakiwa apewe ushauri abadilike. Haiwezekani anapewa pesa kuliko mchezaji yeyote halafu hana msaada wowote kwa timu. Imagine wachezaji key players wengi hawapo lakini wewe unayepata hela zote hizo unakaa benchi dk zote 90.

Unaweza kusema umlaumu kocha kutomuingiza lakini ni ukweli usioweza kupigwa kwamba kocha anaona hatakuwa na msaada wowote kwahiyo ni bora yule aliyechoka uwanjani aendelee tu. Unaona kabisa Jana Kahata kachoka na kazidiwa ila nani aingiee!!

Wito kwa viongozi wa Simba ,huyu bwana apewe ushauri aache utoto.Mashabiki hatutaki mbwembwe na utoto utoto kabisa.

Uongozi pia umpeleke mtu kama Ajibu timu nyingine akapevuke.Hii Simba ni ya kimataifa.Si ya kuja kufanya mzaha.Chonde chonde
 
Kocha kazingua kutomuingiza Morrison.Hakuna uthibitisho wowote kwamba Morrison hasingekuwa na msaada kama angecheza. Kwa Ajibu nakuunga mkono.
 
Usimtetee matola ....hii kesi yake jamaa asingeweza kulazimishaa
Matola hana kosa lolote...Morison kiwango chake ni cha kutilia mashaka mno kwa sasa.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Tulionya humu simba isimsajili hawakusikia,inawezekana ni matatizo yake binafsi au amepigwa misumari
 
taarifa ambazo zipo chini ya kapeti za ndani ya club ya simba zinasema; kwa ss morison hali yake ya kiafyasio njema sana hawez kufanya mazoez magumu, ht mazoezini yy anafanya special program peke yake...
 
Baada ya mechi akaenda kukaa sehemu waliyopo wachezaji wa Yanga. Huyu jamaa atakuwa anashida kichwani.
 
taarifa ambazo zipo chini ya kapeti za ndani ya club ya simba zinasema; kwa ss morison hali yake ya kiafyasio njema sana hawez kufanya mazoez magumu, ht mazoezini yy anafanya special program peke yake...
Hata mwili wake unaonekana umepungua
 
Moja kwa moja kwenye mada.Niseme tu wazi kwamba huyu Morison inatakiwa apewe ushauri abadilike. Haiwezekani anapewa pesa kuliko mchezaji yeyote halafu hana msaada wowote kwa timu.Imagine wachezaji key players wengi hawapo lakini wewe unayepata hela zote hizo unakaa benchi dk zote 90.
Kwa hiyo kwa mtazamo wako ni kwamba anakaa benchi kwa kuwa habadiliki? Point yako hasa sijaipata
 
Mara ya mwisho ulipomuona akicheza kwa kiwango kibovu ni lini na mechi gani?
Jamaa akiacha uigizaji na utoto utoto mwingi ni mchezaji mzuri tu mfumo ukimkubali
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako ni kwamba anakaa benchi kwa kuwa habadiliki? Point yako hasa sijaipata
Yeah...hamshawishi kocha .morison hajitumi na wala haoneshi kabisa kwamba ana kiu ya kupigania nafasi.Ni mara ngapi anaingizwa kwny mechi za Simba anaishia kuboronga tu!!?Lazima kama mchezaji wa nje na anayelipwa kiwango kikubwa cha pesa aoneshe utofauti la sivyo afungashiwe virago
 
Hata mm nimesikia kassim dewji akiongea. BM ana busha[emoji23][emoji23]
Tulishasema vibali vya Morrison tunavyo sisi. Tumevishikilia.... Sasa umemsikia moja wa mabwenyenye wenu anasema Morrison ana Busha inabidi akapasuliwe atakua nje Hadi miezi sita?¿

BONGO NYOSO. HABARI YA MORRISON KWA SOKA LA TANZANIA IMEISHA
 
Yeah...hamshawishi kocha .morison hajitumi na wala haoneshi kabisa kwamba ana kiu ya kupigania nafasi.Ni mara ngapi anaingizwa kwny mechi za Simba anaishia kuboronga tu!!?Lazima kama mchezaji wa nje na anayelipwa kiwango kikubwa cha pesa aoneshe utofauti la sivyo afungashiwe virago
Mimi sikubaliani kwamba akiingia anaboronga, maana hadi mara ya mwisho kuona au kusikia akicheza, alipoingia alichangamsha game. Hata kwa mujibu wa matangazo wali[poenda kule Nigeria dhidi ya Plateau, kama si refa na mshika kibendera kutofautiana, presha ya Morrison ilikuwa izae penati dakika za nyongeza
 
Back
Top Bottom