Simba SC nashauri hizi Mechi zenu tatu za Kirafiki za Kipaumbele kiwe ni Kujiimarisha Kiufundi, Kujifunza na siyo Kushinda

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kwanza nitoe Pongezi nyingi kwa Uongozi wa Simba SC kwa kuamua kutafuta Mechi Tatu Kubwa za Kirafiki za Kimataifa hasa katika Kipindi hiki cha Mapumziko cha Wiki Mbili.

Tarehe 28 August 2022 Simba SC itacheza na Wanaojua Mpira Asante Kotoko huko nchini Sudan.

Tarehe 31 August 2022 Simba SC itacheza na Mafundi wa Mpira Al Hilal huko nchini Sudan.

Na tarehe 3 Septemba 2022 Simba SC itacheza na Wataalam wa Mpira As Arta Solar hapa nchini Tanzania.

Wakati Timu nyingine ya Tanzania iliyowekeza Kumfunga tu Simba SC Kiuchawi na kutoa Mikafara ikijiandaa nayo Kucheza Mechi zake za Kirafiki za Kimataifa na Vilabu vyepesi halafu hapa hapa Dar es Salaam Tanzania ( kwakuwa hawana Nauli za kutoka Nje' ya Tanzania ) nashauri yafuatayo kwa Simba SC kuelekea hizi Mechi zao Tatu Kubwa za Kimataifa.

Nashauri Kipaumbele Kikuu katika hizi Mechi zote Tatu ziwe ni za Kukiunganisha zaidi Kikosi.

Nashauri Kipaumbele Kikuu katika hizi Mechi zote Tatu ziwe ni Kurekebisha Makosa Makuu yanayoitesa Simba SC hasa ya Umakini wa Kukaba na Kucheza Mipira ya Juu.

Nashauri Kipaumbele Kikuu katika hizi Mechi zote Tatu kiwe ni Kukijenga zaidi Kikosi hasa katika Safu ya Ushambuliaji ambayo inatengeneza nafasi nyingi ila haizitumii ipasavyo Ili Simba SC iwe inashinda Goli nyingi.

Nashauri Kipaumbele Kikuu katika hizi Mechi zote Tatu kamwe kisiwe ni Kushinda ( tena kwa Kuhonga ) Ili Kutudanganya Mashabiki bali tuzitumie hizi Mechi katika Kujisahihisha na Kujiimarisha Kimbinu na Kiufundi.

Binafsi nitafurahi hata kama Mechi hizi zote Simba SC tutafungwa au tutatoka Sare zote Ili mradi tu ziwe zimetuongezea Faida nyingi Kimichezo.

Kuna Timu Moja nchini Tanzania ambayo haina Uzoefu wa Kucheza Mechi za Kimataifa na ina Ubobezi wa Kucheza Mechi Moja tu ya Ndani na Ugenini kisha inafurumushwa Mashindanoni yenyewe imepanga Kucheza Mechi zake za Kirafiki za Kimataifa na Vilabu vya hovyo hovyo Ili Ivihonge iweze Kushinda Mechi zote hizo kisha Kuwaaminisha Kiuwongo Mashabiki wake kuwa wako Imara kwa Michezo ya Kimataifa wakati tunaowajua tunajua kuwa watafurumushwa ( wataondoshwa ) katika Mchezo wao Mmoja tu.

Hakikisha Unasensabika Leo sawa?
 
Hahahaha haaaaaaa hahahaha we jamaa.
 
Bora wamechagua timu zinazojulikana kidogo sio wale madereva tax waliokuwa wakicheza nao pre-seson.
 
Nyie mmewachagua nani pale utopoloni?

Hivi kila kitu mfundishwe na Simba SC kila siku mpaka lini?
 
Unajiandaa kisaikolojia hata ikitokea mmepigwa dosen ya magoli mtuambie mlikuwa mnarekebisha makosa dhahili hata draw hampati katika hizo mechi.
Hizi Ni friendly match kuimarisha vikosi na makocha kutest mifumo yao. Kuangalia uwezo wa kupambana na washindani walio bora ili kujua uwezo wako na kujiimarisha.Siyo mechi za kutafuta matokeo.

Tunaamini Asante Kotoko na Al Hilal watakuwa kipimo kizuri na sahihi kwa Simba.

Muwe mnaongea mpira na siyo Kila kitu Ni ushabiki maandazi.
 
Bora wamechagua timu zinazojulikana kidogo sio wale madereva tax waliokuwa wakicheza nao pre-seson.
Hizi Ndiyo akili ndogo.

Yanga ilicheza na Friends Rangers kwahiyo hii timu ya ndondo Ndiyo bora.

Wenye akili utopoloni Ni wawili tu, Kikwete na mzee Manara, alisikika chizi mmoja.
 
Kitaalamu siku 42/50 zinatosha Kwa kocha kutathmini na kujua uelekeo au uwezo wa timu husika. Fikiria Kwa Simba ya miaka mitatu nyuma ilikua na kikosi imara kuliko Cha Sasa na bado ilihitaji kupulizia madawa vyumba vya timu pinzani.
Bado Simba ilihitaji kuhonga Marefa, kufukia makafara na kuwasha moto wa kishirikina uwanjani Ili ipate matokeo.
Sasa Simba iliyopo mbakaleo kocha anakaribia miezi miwili haijapata first eleven na Kuna baadhi ya mbumbumbu Wana amini ikicheza mechi tatu itakua tayari Kwa ushindani kimataifa.
Inatakiwa mkubali Simba imechemka vibaya katika usajili.
 
Unajiandaa kisaikolojia hata ikitokea mmepigwa dosen ya magoli mtuambie mlikuwa mnarekebisha makosa dhahili hata draw hampati katika hizo mechi.
Huwa mnajiaminisha hivi, baadae Simba Sc ikishinda mnaanza kusingizia kuwa imekutana na vibonde.
 
Back
Top Bottom