Simba SC Nawapenda mno, ila kwa hili mtanisamehe kwani nahisi kuna tatizo mahala

Simba SC Nawapenda mno, ila kwa hili mtanisamehe kwani nahisi kuna tatizo mahala

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Tokea GENTAMYCINE nizaliwe na niwe mfuatiliaji wa Mpira hadi sijawahi ama Kuona au Kusikia Klabu inakwenda Pre Season Kimafungu Mafungu kama ilivyo kwa Klabu yangu pendwa ya Simba SC.

Kwa mtazamo wangu sioni Aibu kusema kuwa Simba SC yangu haijaenda Pre Season kama wasemavyo Wao ila imeenda Pre Season and Tourism in Turkey kutokana na disorganization iliyoko japo kws sasa inafichwa kwa Sajili Kubwa Kubwa zinazofanyika.

Kwa Maoni yangu Simba SC imeenda tu kupoteza muda huko nchini Uturuki na badala yake naona kama ingebakia hapa hapa nchini Tanzania na Mipango pamoja na Mikakati kuwekwa Timu ingepata Pre Season Bora kabisa na yenye Tija.

GENTAMIYCINE nakiri kuwa Yanga SC siipendi na hata Mashabiki wao hapa JamiiForums wanalijua hili ila sitaki kuwa Mnafiki maamuzi ya Yanga SC kubakia hapa hapa Tanzania kwa Pre Season yao kuna Faida Kubwa Kiufundi, Kisaikolojia na Kimaandalizi hali ambayo itawapelekea Kufanya vyema Kimchezo na Kimafanikio ( Kimatokeo ) kisha kama kawaida yetu wana Simba SC ( akina GENTAMIYCINE na SAGAI GALGANO ) tutaanza kusema Yanga SC wanahonga na Kununua Mechi.

Haiwezekani na haiingii Akilini yaani Timu iko Uturuki Kimafungu Mafungu, Msemaji yuko Dar es Salaam, Jezi zimeenda Kugandishwa Kileleni Mlima Kilimanjaro na Kocha Mkuu Robertinho yuko Kwao Brazil. Yaani ni Vululu Vululu tupu tu.

Ukiwa na Akili timamu, huna Unafiki na Ushabiki wa Kishamba na Kipumbavu kwa mapungufu haya GENTAMYCINE niliyoyaainisha hapa utakubaliana nami kwa 100% kuwa kuna Shida Kubwa katika Management na Administration ya Klabu ya Simba.

Mapungufu haya yasijirudie tena.
 
Logic sana mpangilio haujakaa watu wengi muhimu hawapo kwenye eneo muhimu zaidi
Jezi ilipaswa kuwa tayari inatumika turkey
Msemaji alipaswa kuwa turkey
Kocha alipaswa kuwepo
Wachezaji walipaswa kuwepo angalau 95%
Anyway kama ulivyosema Kuna kitu hakiko sawa
 
Logic sana mpangilio haujakaa watu wengi muhimu hawapo kwenye eneo muhimu zaidi
Jezi ilipaswa kuwa tayari inatumika turkey
Msemaji alipaswa kuwa turkey
Kocha alipaswa kuwepo
Wachezaji walipaswa kuwepo angalau 95%
Anyway kama ulivyosema Kuna kitu hakiko sawa
Hii pre season hawakuipanga vyema....walikurupuka
 
Back
Top Bottom