Simba SC Nawapenda mno, ila kwa hili mtanisamehe kwani nahisi kuna tatizo mahala

Simba SC Nawapenda mno, ila kwa hili mtanisamehe kwani nahisi kuna tatizo mahala

Nilikuwaga mshabiki wa Simba kindakindaki lakini baadae nkajagundua ni ujinga, ninayo Mambo ya muhimu zaidi kudeal nayo kuliko kuifuatilia Simba sana. Mara moja moja sana kuifuatilia Simba.
 
Simba bado haijajipanga mambo mengi wanakurupuka Yanga wapo vizuri sana wanapanga mambo yao kitaalamu zaidi tusubiri ngao ya hisani ndio watu watajua ubora na mipango ya Yanga inavyolipa
Friends of simba ndio adui nambari wani wa Simba
 
Tokea GENTAMYCINE nizaliwe na niwe mfuatiliaji wa Mpira hadi sijawahi ama Kuona au Kusikia Klabu inakwenda Pre Season Kimafungu Mafungu kama ilivyo kwa Klabu yangu pendwa ya Simba SC.

Kwa mtazamo wangu sioni Aibu kusema kuwa Simba SC yangu haijaenda Pre Season kama wasemavyo Wao ila imeenda Pre Season and Tourism in Turkey kutokana na disorganization iliyoko japo kws sasa inafichwa kwa Sajili Kubwa Kubwa zinazofanyika.

Kwa Maoni yangu Simba SC imeenda tu kupoteza muda huko nchini Uturuki na badala yake naona kama ingebakia hapa hapa nchini Tanzania na Mipango pamoja na Mikakati kuwekwa Timu ingepata Pre Season Bora kabisa na yenye Tija.

GENTAMIYCINE nakiri kuwa Yanga SC siipendi na hata Mashabiki wao hapa JamiiForums wanalijua hili ila sitaki kuwa Mnafiki maamuzi ya Yanga SC kubakia hapa hapa Tanzania kwa Pre Season yao kuna Faida Kubwa Kiufundi, Kisaikolojia na Kimaandalizi hali ambayo itawapelekea Kufanya vyema Kimchezo na Kimafanikio ( Kimatokeo ) kisha kama kawaida yetu wana Simba SC ( akina GENTAMIYCINE na SAGAI GALGANO ) tutaanza kusema Yanga SC wanahonga na Kununua Mechi.

Haiwezekani na haiingii Akilini yaani Timu iko Uturuki Kimafungu Mafungu, Msemaji yuko Dar es Salaam, Jezi zimeenda Kugandishwa Kileleni Mlima Kilimanjaro na Kocha Mkuu Robertinho yuko Kwao Brazil. Yaani ni Vululu Vululu tupu tu.

Ukiwa na Akili timamu, huna Unafiki na Ushabiki wa Kishamba na Kipumbavu kwa mapungufu haya GENTAMYCINE niliyoyaainisha hapa utakubaliana nami kwa 100% kuwa kuna Shida Kubwa katika Management na Administration ya Klabu ya Simba.

Mapungufu haya yasijirudie tena.
We jamaa nishakujua. Kwa uandishi huu wewe ni mtoto wa mzee Sandey. Unatusumbua instagram kule
 
Ndo kwanza hata ngao ya jamii hamjapasuka.Muda ni mwalimu mzuri
 
Uongozi wa Jamiiforum waangalie namna ya kuweka sheria kuwa kuanzisha nyuzi mwisho ni nyuzi tatu kwa siku la sivyo kuna machizi kama chizi wa uzi huu hawana break katika kuanzisha nyuzi.
 
Ukiwa serious na soka la Bongo utajiumiza Bure.

VIONGOZI wengi ni Mburura, ZUMBUKUKU.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Me nilishaacha kuumiza kichwa na soka la bongo nawaangalia tu
 
Back
Top Bottom