SIMBA SC: Tangu tuanze kampeni ya kuchangia ujenzi wa uwanja tumekusanya Tsh Mil 60 hadi sasa

Ukinambia million 60 siwaelewi kabisa,

Maana Nakumbuka MO dewj ndo alikua mtu wa kwanza kabisa kuchangia uwanja, yeye pekee alichangia billion 2.

Hizo pesa zilikwenda wapi?[emoji848]
Unatafuta matusi🤣🤣
 
Hatuwez kuwa klabu kubwa yenye kuheshimika Africa Kama hatuna kiwanja cha kimataifa tena wangetengeneza sports arena kabisa watanzania tuchangie maendeleo
 
Milion 60 wakimaanisha pesa walizochanga mashabiki
Hii inatosha kusafisha eneo ambalo unatakiwa uwanja ujengwe🤣🤣🤣🤣 wabongo like serious 60 million aise mie kama ningekuwa mo wala sitoi hela yangu
 
Hivi ile fine ya 23m ya CAF walishailipa? Iseje kuwa wamelipa ya ndugu na dada zetu!
 
Inawezekana wote tulio comments hapa hatujachanga, harafu tunalaumu watu
 
MIEZI SITA MILIONI SITINI.

Namba 6 yenye utata.
✍️Miezi 6 iliyopita Simba SC ilianzisha kampeni ya kuchangia Uwanja.
✍️ Imechukua miezi 6 hesabu kuwekwa bayana.
✍️Milioni 60000000 zimechangwa kwa miezi SITA ikiwa ni Sawa na uwiano wa Milioni 10 kwa Mwezi.
✍️Wale watu wa kukokotoa tusaidiane kidogo: Tukichukua tu kiasi Cha buku kama kiwango Cha chini Cha mchango kwa waliochangia Mimi nikiwemo, basi Ina maaana ni Simba SC Ina mashabiki elfu sitini TU ambao Ndio waliochangia.KWELI? Sasa si afadhali kutengeneza mechi ya bonanza na Timu Moja Afrika mashariki,kuifanyia promo mechi hiyo na kuujaza Uwanja kwa kiingilio Cha 5000 tu utakuwa umekusanya 5000×60000=300,000,000(milioni mia tatu) ukitoa gharama za uwanja na gharama za timu alikwa unaweza ukabakia na Milioni 240,000,000 ambayo kwa hesabu tuliyopewa na klabu yetu leo basi tunahitaji miaka 6 kuchangia milioni mia tatu achilia mbali bilioni 30 zanazihitajika kujenga Uwanja. Je si tutahutaji miaka 60 Tena ya uhuru?
✍️Vipi na zile bilioni mbili (2,000,000,000) alizoahidi mdhamini wetu kuwa ameweka katika kuendeleza mchango huu uwanja? Mbona hazikujumuishwa katika taarifa ya Leo? Au Mimi sikuelewa? Au hatupaswi kuhoji?
✍️Kwa hiyo mnataka kutuaminisha kuwa Simba hii iliyo na wapenzi wengi iwe ni watu elfu 60000 tu ndio wamechangia? NATAFAKARI.
✍️Itoshe kusema majibu hayakujitosheleza na haikuwa na haja ya kulizungumzia hili. TUMEPIGWA.
✍️Kwanini kusiwepo na update ya Kila Mwezi kuhusu zoezi lile ikawa unapata ujumbe kila unapochangia kuwa 'Mchango wako umefikia mtu wa....au namba.....)? NAWAZA KIMOYOMOYO

Kama ilivyo kwa simba hata kwa Yanga endapo utaratibu itakuwa ni huu wa kuficha taarifa za makusanyo hasa kutoka kwa wanaochangia basi NANI ZAIDI itageuka na kuwa ZAIDI NI NINI Mbona mchango umedorora?
 
Inamana ile Bil 1 aliyoitoa Mudi sikua anaanzisha hii hamasa ya kuchangia ilikuwa maneno tu!!
 
Duh sina wasiwasi na Simba kuhusu hela iliyopatikana ila dalili zinaonyesha ni ngumu kujenga uwanja kwa michango,kama mwekezaji hatajenga basi uwanja sisi mashabiki hatuwezi ,maana tunazidiwa na mchango wa sadaka ya mwamposa kwa jumapili mbili
 
Wazee wakuiga yanga vilaza
Waliponda simba day wakaiga
Wakaponda mchango wa uwanja sasa hivi wanakuja huko huko yanga mwenye akili ni kikwete na mzee Sunday manara wengine wote wanasubiria simba waanzishe project waige.
 
Labda wameondoa 00 kwenye hizo tarakimu!
 
Umesahau labda. Siku mwinyi zahera anakuja kumkomboa Yule kipa wenu mkongo Kindoki kwa mamantilie pale kamanga feli Mwanza kutokana na msosi wa buku mbili na nusu aliokula kwa huyo mamantilie umesahau?
Kama vipi lete huo ushaidi wa Kindoki nami nilete ushaidi wa Kaduguda akilalamikia hela zake za chapati alizowanunulia wachezaji wa Simba kipindi kilee, shida yenu mnajisahaulisha.
 
Viongozi wa Simba wanatakiwa wawe makini sana.
Sio kila anayesema yeye Simba anaipenda Sana Simba
Kuna mambo ya mgongano wa kimaslahi.
Kuna wazee wameshaanza kuibuka kumpinga Barbara.
Timu imefanya vizuri miaka 4 Leo kuteleza kidogo wameanza maneno maneno
unaeza kuta hata mleta uzi hajachanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…