Simba SC tujiandae kujenga timu ya baadae kwa sasa wachezaj wamechoka

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Ukiangalia SImba kwa nini timu haitembee. Kuna mambo mawili ya kuangalia kwanza UMRI wa wachezaji waliopo SIMBA wengi ni 30 and above, Pili SImba haipandishi vijana wa under 20 kuja timu ya wakubwa.
1. SIMBA hii imecheza CAF CL na CAF CC kwa muda wa miaka kama minne mfulululizo ikiwa na hawa watu
MANULA, KAPOMBE, ZIMBWE JR, BOCCO, NYONI, MKUDE, CHAMA na MZAMIRU

Hawa wote hawana mbadala wa umri chini ya miaka 21 na 20 ni kwa sbb simba inataka mafanikio haaka haraka bila kuandaaa wachezaj ambao wangeweza kuingia hata dk 85 mkiwa mmeshinda goli 4 au 3 bila ili kuwapa confidence hii ndio leo tunabaki kushikana uchawi na kugombana.

Kwa hiyo Viongozi wa SIMBA wapate mtu wa mpira ndani ya uongozi TECHNICAL DIRECTOR ili awatengeneze muundo mzuri ambao tutaenda nao miaka 5 ijayo tena badala ya kuanza kushikana uchawi na matusi. Mpira yes ni kuwekeza wanaosema simba imeshindwa kusajili....changamoto ipo kumpata mchezaji kama beki wa petro de luanda au mamelod lazima utoe 2b au 1b je SIMBA ina hela hiyoooo?

2. Kwangu me nafikiria viongozi kama kweli wana nia ya kuirudisha SIMBA pazuri tuinvest kwa kina
BANDA ISRAEL MUSSA na wachezaj kama baleke tusiwatupe....tulete vijana kama akina nashon vijana wa ktz kama watatu tuanze kuwapa nafasi dk zikiwa zimeisha ili hawa 30 ages wakiondoka tuwe na timu imara. Kununua tu sio big deal kununua ni kama KUBET unaweza kumleta mchezaji SIMBA akawa GALASA wakati kule alikuwa mzuri mara ngapi yanga nao wamenunua wachezaj hawaperform ni kwamba wamebahatisha kwa MAYELE BANGALA NA MOLOKO lakini tumeona bigirimana kambole sasa hv beki lao la mali hamna kitu kwa hiyo SISI kama simba Viongozi wawe na jicho la mpira hawa RAJA MAMELOD na WYDAD hawanunui wachezaj wote bali wananunua wachezaj wawili au mmoja wengi ni kutoka hapo hapo U20 waliopikwa hapo hapo.


VIONGOZI SOMENI HII NA MUIFANYIE KAZI.


SIMBA NGUVU MOJA
 
Kuwekeza kwa under20 hakuna percent ya mshahata hawawezi kukuelewa
 
Sahihi

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 


Sijui kwanini uwa hawafanyi ivii (kuwapa dakika za kucheza walau dk 15 - 20 za mwisho)kwa wachezaji wao makinda na wale wasiopata nafasi ili kuwapa confidence !?

Unakuta timu inaongoza 3+ dk ya 70 Bado wanang'ang'ana na wachezaji haohao, matokeo yake kwenye unapaswa kufanya rotation ya wachezaji unashindwa kufanya ivyo, kwasababu ukuwa unawapa nafasi ya kucheza wachezaji waliopo benchi. Mfano mzuri ni wiki hii wenzao Yanga mechi hii ktkt ya wiki waliweza badilisha wachezaji 9 walioanza zidi ya TP Mazembe kuwapumzisha lakini wao Simba iliwawia vigumu kutokana na ufinyu wa Kikosi wanao usababisha wao mwenyewe.
 
Ukiondoa kuchoka, pia wachezaji wengi umri umewatupa. Na mchezaji mwenye umri mkubwa, na kasi yake pia uwanjani hupungua! Na majeraha muda wote humuandama.
Ni vizuri tujifunze kusajili wachezaji watakaotupa huduma kwa muda mrefu.
 
Ni vizuri tujifunze kusajili wachezaji watakaotupa huduma kwa muda mrefu.
kama akina Denis Nkane na Clement Mzize wa Yanga, ni vijana kabisa na wakisajiliwa wataingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza, na watatupa huduma kwa muda mrefu
 
kama akina Denis Nkane na Clement Mzize wa Yanga, ni vijana kabisa na wakisajiliwa wataingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza, na watatupa huduma kwa muda mrefu
Hata kina gadiel na sawa dogo ni project itakayo tulipa mbeleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…