Mpira huwa na matokeo ya KIKATILI sana. Nadhani wadau wa soka tujiandae kisaikolojia, maisha sio marahisi kama jinsi tunavyowaza.
Tujiulize Simba ilifika je hapa kwenye michuano hii. Tulifanyiwa Surprise moja ya ajabu pale LUPASO, hakuna aliyeamini.
Hiyo team yenyewe tunajua ilipo now? Galaxy inashika mkia kwenye kundi lake na ni lazima itoke. Hii ni ishara kwamba simba inakuzwa na kelele na ma promotion yasiyo na tija, reality on the ground ni tofauti kabisa.
Asec inakikosi kizuri, mchezaji mwenye umri mkubwa pale ni miaka 22 , wapo energetic , young and smart, kile kikosi next FY kitakuwa ni moto.
Simba Ina changamoto nyingi, kuanzia kocha , kocha pablo hana psychological tags za kufundisha Africa, hilo ni tatizo moja wapo, Tatizo lingine ni Simba kuamini katika ujinga, huwezi kuwa timu ya ushindani na striker kama Kagere , au Mugalu , ni kupoteza muda.
Hakuna mpira wa inshallah inshallah, mpira ni Investment. Uki invest Vyema , likelihood ya kufika mbali ni kubwa.
Naishauri Simba ifanye usajili wenye tija na kuacha fantasy za mitandao au ushindani wa kugombea wachezaji na Yanga , ni ujinga.
Nendeni west Africa huko Burkinafaso, Ghana, Ivory’s Cost , Cameroon , kuna vitoto vipo safi na wana miili mizuri na wana Nature za kimpira.... acheni kukomaa na watu wazeee , mnatoa expectation kubwa kwa mashabiki halafu uhalisia ni kubahatisha.
Hata ile timu ya Morocco , hamkuifunga, ukweli ni kwamba Mlifungwa But fitna ilitawala.
Kufungwa na Asec Goli 3 na Penati 2 , huo ndio uwezo wenu, vile vitoto vingi ni under 20 vina spirit na ndoto za ku Excel soka lao la kulipwa huko ulaya.
Yaani hata Simba ikifika Robo fainali, asilimia 95% , hapo ndio itakuwa ni mwisho wao. Hakuna kikosi cha kucheza nusu fainali.
Pamoja na yote , Simba ana asilimia 55 ya kwenda mbele. Asec ana asilimia 50 ya kwenda mbele , BERKANE Ana asilimia 55 ya kwenda mbele, GENDERMARIE ana asilimia 15 ya kwenda mbele , pamoja na uchache wake, ni wazi wanaweza kumbania Mnyama asipite, yaani any suluhu, Simba Out.