Simba SC v Young Africans SC

Kuna uzi nomeuona kuna mtu kasema leo atajing'ata 'MATAKONI'endapo timu yake itachezea kichapo.
 
Kumbe tunaweza ongea biashara, hayo mashimo bado yanapatikana kwa urahisi huko Geita?

Mengi lakini siku hizi jamaa wajanja sana wanataka 50/50 sasa kazi ipo,siku hizi tumebadili mwelekeo kidogo tunachenjua tu hiyo ndio babu kubwa kwa sasa mkuu.
 
Mengi lakini siku hizi jamaa wajanja sana wanataka 50/50 sasa kazi ipo,siku hizi tumebadili mwelekeo kidogo tunachenjua tu hiyo ndio babu kubwa kwa sasa mkuu.
Mbona unaongea lugha ngumu, kuchenjua ndo kufanyaje?
 
Kaka mandieta kauli kama hizi huwa sio nzuri sana kuna jamaa alikula BAN humu siku yanga anaua mtu 3 hivi hivi,sasa na wewe angalia ka sababu ukishindwa kujing'ata utang'atwa,by the way Yanga ndiye mshindi leo ingawa sitaki kuapia chochote Mkuu.
Mkuu heshma yako! Najua leo huwezi apa kwakuogopa history.
 
Leo nita shangilia Simba kwa mkopo nikitokea Azam, na ndio mechi yangu ya kwanza (tangu nazaliwa) kumshangilia mnyama, kwahiyo naomba Simba usini dhalilishe na usilete za Libolo. Kila la kheri mnyama.
 
Mbona unaongea lugha ngumu, kuchenjua ndo kufanyaje?

Jamaa yangu Masuke hizi lugha zinapatikana sana kwenye masuala ya Madini,ukimuuliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Steven Masele anajua sana,kwa faida yako tu kwa sababu unataka kujua hii ni kuvundika ule mchanga wa dhahabu,acha mawe,mchanga ambao umetokana na mawe yaliyotwangwa na kusagwa kisha kuoshwa na kutolewa kwa dhahabu,sasa unachukuwa ule mchanga unauvundika kwa kutumia sumu ya Cynide,halafu unakwenda kuchoma unakomba dhahabu yote na hii ni njia nzuri sana kwa sasa imetajirisha wengine sana na hasa katika ukanda wa ziwa victoria,kama unamkumbuka yule mzungu aliyekamatwa sehemu moja Nyarugusu kwa tuhuma za kutorosha dhahabu,mimi aliniajiri na nikajifunzia hapo nikanzisha ya kwangu jamaa yangu ni kweli yule mzungu ameibia sana serikali zamanai tulikuwa tunakimbilia mawe lakini kumbe ile kitu ni hatari sana.

Kama vipi tukutane uwanjani tuongee kwa kirefu zaidi kama unaweza naweza kukuajiri kwa sababu ile kazi ni ngumu kwa hiyo na mshahara ni mkubwa.mwezi ujao nafungua mgodi mwingine wa uchenjuaji kule maeneo ya Misungwi,hii biashara kuna vigogo wengi sana wa serikali hivi sasa wanaifanya,wapo wengi mpaka mawaziri,waliokuwa mawaziri,watoto wa vigogo!.
 

du!!! Hii match leo inatoa na watu,hya mkuu,tuombe leo tukabidhiwe kombe tukiwa tumempga mnyama hata 6!!
 
Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi, bahati mbaya leo sitakuwepo uwanjani, itabidi tuwasiliane zaidi kama nitaona inafaa unipe hiyo ajira.
 
Kikosi kazi cha yanga ndio tupo njiani tunakuja na msafara wetu
 
Sina amani, kuna dalili za kusherehekea harusi na vitambaa vyeusi mkononi.
 
Kama Ngassa anacheza,uwezekano wa Simba kupigwa 6 upo sana!maana hajitambui huyu kijana!ataisumbuaje timu anayohamia msimu ujao?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Niko uwanjani taifa mashabiki kama nyuki na kwa jinsi vuvuzela zinavyolia ni Yaangaaa oyeeeeeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…