Simba SC v Young Africans SC

Simba SC v Young Africans SC

Wakuu hakuna chanel ya bongo itakayoonyesha mechi hii?
 
Mkuu kama hauna access mi nitakuwa nawapa raha. Kiongozi wangu Akilimali kasema leo ushindi upo.
Fidel80, nakuaminia mkuu, lakini usitukimbie yanga wakifungwa...
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha haah!! Nipo hapa Makuti Morogoro, nimechelewa usafiri wa kuja taifa.......nitafuatilia kupitia hapa JF. Nategeme utarusha live mkuu na wadau wengine.

Kama upo makuti mwone Aisha hapo akuhudumie natuma mpunga kwa m pesa itakusaidia kutopata presha
 
Leo nimeamua kusikiliza radio ya CCM, kweli kila kitu kina faida na hasara, leo naona faida ya CCM kuwa na radio, nimehangaika kutafuta radio yoyote iliyo online inayotangaza hii mechi; nimeanzia TBC Taifa bila bila, Kiss FM bila bila, Radio One hakuna kitu, cha kushangaza radio ya CCM imeniokoa. Leo ndo nimefaidi kodi yangu inayoenda CCM kama ruzuku.
 
Hahaha thutubu mi nitatiririka Live hapa mwone shemeji yako Aisha ila usimtongoze.
ha ha ha haaah!! Mkuu haya ngoja nimtafute huyo Aisha nianze kupiga Kinana Lager taratibu, huku nikisikilizia huko taifa...
 
Full nyuki,full nundu,mtu nyomi taifa aise.
Wachezaji wanapasha misuri yao sasa.Pia naona Wachezaji wa Simba wanakizunguka kibendera cha kona.
 
Haki ya mama yangu mzazi sijawahi kuona uwanja wa Taifa umejaaa kiasi hiki,ndio kwanza natinga ndani ya uwanja huu,robo tatu ya uwanja umesheheni rangi ya njano,kijani na nyeusi.
 
Leo nimeamua kusikiliza radio ya CCM, kweli kila kitu kina faida na hasara, leo naona faida ya CCM kuwa na radio, nimehangaika kutafuta radio yoyote iliyo online inayotangaza hii mechi; nimeanzia TBC Taifa bila bila, Kiss FM bila bila, Radio One hakuna kitu, cha kushangaza radio ya CCM imeniokoa. Leo ndo nimefaidi kodi yangu inayoenda CCM kama ruzuku.

ah ah ah, mkuu kumbe wakitoka madarakan utawamic sana!
 
Back
Top Bottom