Simba SC vs El Merreikh kuchezwa bila mashabiki

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara leo ametangaza kuwa CAF wamezuia Mashabiki kwenye mchezo wa Club Bingwa Afrika March 16, 2021 Uwanja wa Mkapa kati ya Simba vs El Merreikh ya Sudan hivyo Mechi hiyo itachezwa bila Mashabiki .​




Haji manara

Mechi yetu na Al Merrikh ipo pale pale lakini wakati tukiendelea na maandalizi tumepokea taarifa kutoka TFF ambayo imetolewa na CAF kwamba tucheze bila mashabiki .

" " Mnawajua mashabiki wetu lakini hakuna namna tutacheza bila mashabiki . Wanaruhusiwa maafisa na watu wachache ambao wanahusika na mchezo . "

" Simba imezoea kucheza bila mashabiki ikiwa nje ya nchi lakini sikumbuki kama hapa nchini tumewahi kucheza bila mashabiki .

Tunawaomba radhi mashabiki kwa mechi hii sababu ni maamuzi ya CAF ambao ndio wenye mamlaka ya soka Afrika . "

" Itakuwa ni vita ya kimya kimya kama ambavyo Simba anawinda . Wachezaji wetu wamezoea kucheza mbele ya mashabiki na wamezoea kucheza bila mashabiki , naamini wana uzoefu wa kutosha kucheza kwenye hali kama hiyo .

" - Haji Manara Afisa habari wa Simba
 
Duuh yule aliokua anasema mechi zichezwe na mashabiki yuko wapi awakemee hawa CAF kwasababu mechi inachezwa hapa kwetu na walipaswa wafuate misingi ya hapa kwetu ikiwrmo mashabiki kuwa na risiti ya kutoka muhimbili baada ya kupiga nyungu kwenye mashine iliozinduliwa na Hospital kuu ya taifa chimbuko la madaktari bingwa hapa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…