TEAM 666
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 4,399
- 8,594
Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara leo ametangaza kuwa CAF wamezuia Mashabiki kwenye mchezo wa Club Bingwa Afrika March 16, 2021 Uwanja wa Mkapa kati ya Simba vs El Merreikh ya Sudan hivyo Mechi hiyo itachezwa bila Mashabiki .
Haji manara
Mechi yetu na Al Merrikh ipo pale pale lakini wakati tukiendelea na maandalizi tumepokea taarifa kutoka TFF ambayo imetolewa na CAF kwamba tucheze bila mashabiki .
" " Mnawajua mashabiki wetu lakini hakuna namna tutacheza bila mashabiki . Wanaruhusiwa maafisa na watu wachache ambao wanahusika na mchezo . "
" Simba imezoea kucheza bila mashabiki ikiwa nje ya nchi lakini sikumbuki kama hapa nchini tumewahi kucheza bila mashabiki .
Tunawaomba radhi mashabiki kwa mechi hii sababu ni maamuzi ya CAF ambao ndio wenye mamlaka ya soka Afrika . "
" Itakuwa ni vita ya kimya kimya kama ambavyo Simba anawinda . Wachezaji wetu wamezoea kucheza mbele ya mashabiki na wamezoea kucheza bila mashabiki , naamini wana uzoefu wa kutosha kucheza kwenye hali kama hiyo .
" - Haji Manara Afisa habari wa Simba