Simba SC wageukia Madhabahu. Wamuomba Mtume Mwamposa "ahudhurie" mchezo wa tarehe 9/04

Simba SC wageukia Madhabahu. Wamuomba Mtume Mwamposa "ahudhurie" mchezo wa tarehe 9/04

mechi ijayo ya tarehe 9/04/2025
Hii mechi itakua moja ya mechi mbaya sana kwa upande wa Simba

Niwashauri km wanaweza kutumia mbinu waliyokimbia kipigo kwa Yanga kwamba uwanja sijui umefanyaje na awamu hii basi watumie mbinu ile ile nawahakikishia TFF na Bodi ya Ligi watakua upande wao lazima wataahirisha mechi na mchezo hautochezwa hio tarehe 9

Maana wakienda kucheza lazima tu watachapwa tena watachapwa sana bora hata zile 2 walizochapwa kule ila huku watachapwa mpaka aibu, na kuhusu Bwana Mwamposa namshauri siku hio asikanyage uwanjani maana ataondoka na aibu ya kushuhudia mashabiki wa Simba wanavyong'oa Viti na kuwarushia mashabiki wa timu pinzani

Ushauri kwa bodi ya Ligi na TFF ninaomba mashabiki wa Simba upande watakao kaa basi vile viti viondolewe vyote wakalie zege la sivyo likitokea lolote lawama zirudi kwao maana tulikwisha watahadharisha mashabiki wa Simba lazima wataondoka na Viti vya uwanja
 
Katika ibada ya Leo tarehe 6/04, Mtume Boniphace Mwamposa amekiri kupokea mualiko wa Simba SC kuhudhuria na kuwaombea kuhusu mechi ijayo ya tarehe 9/04/2025.

Ameahidi kuhudhuria au kutuma wawakilishi katika mechi hiyo na atawaombea.

Hongereni Simba SC kwa kuachana na Matunguli. Shikilieni hapo hapo.
Washapigwa mapema sana.
 
Mwaposa sio poyoyo waku side na timu itakayofungwa...hawezi kushusha Brand yake, eti ameiombea Simba isichapwe alafu inachapika...akikanyaga kwa Mkapa nile BAN ya siku 3 😂.
 
Acha nicheke🤣🤣

Lini wameachana na tunguli. Wanachanganya vyote. Hapo wamealika waganga, vile vizee vifupi na mbuzi zao, wachungaji na mashekhe. Hiyo siku itakuwa siku ya kuvunja na wengine wanaunga.
Nahisi uliwahi kuugua kifafa. Hivi hiyo stori ya vizee vifupi na mbuzi kumbe uliiamini, utakuwa huna akili.
 
Nahisi uliwahi kuugua kifafa. Hivi hiyo stori ya vizee vifupi na mbuzi kumbe uliiamini, utakuwa huna akili.
Ndio shida ya watu mliokulia na kuishi milembe ni ngumu kujua wenye akili wanakuwaje kila jambo mnachukulia seriously wakati hamko serious 🤣🤣
 
Kutokea enzi na enzi, Simba ndiyo baraka ya Mungu kwa mpira wa Tanzania. Kila wakati Mungu akitaka kuibariki Tanzania kwenye mpira anaitumia Simba.
Anaibariki vipi timu inayowanga hadharani nchi za watu
 
Mkuu respect sana kwako, unaonekana mstaarabu sana kwenye haya maswala ya usimba na uyanga naonaga Jinsi unavyotoa koment zako kwa staha, na unaonekana uko vizuri kiuchumi na huna muda na ushabiki wa kijinga wenye matusi na lugha chafu na za fedheha.
Shukrani sana mkuu I appreciate you
 
Mkuu respect sana kwako, unaonekana mstaarabu sana kwenye haya maswala ya usimba na uyanga naonaga Jinsi unavyotoa koment zako kwa staha, na unaonekana uko vizuri kiuchumi na huna muda na ushabiki wa kijinga wenye matusi na lugha chafu na za fedheha.
Duuu hapa kuna mtu anatengenezewa mazingira yakizinga pameanza kuchangamka
 
Sitaki kuamini kuwa viongozi wamemuita Mwamposa awaombee. Na kama viongozi wamefanya hivyo basi Simba itakuwa haina viongozi kabisa bali itakuwa inaongozwa na watu wasiojua kuwa mpira ni sayansi. Shida ya Simba sio kuombewa bali wiki nzima ilitakiwa benchi la ufundi lihangaike na safu yao mbovu ya ushambuliaji kwani walikosa magoli zaidi ya matano ya wazi kabisa tena ugenini pamoja na "half chances" zisizo na hesabu. Na la ziada wangetafutwa watu wa saikolojia ili wawe na "session" na wachezaji kabla ya mchezo wa marudiano ili wachezaji wawe na utulivu. Kwa sababu kitakachowatoa Simba au kuwafanya wasonge mbele kwenye mechi ya marudiano ni kitu kimoja tu kati ya utulivu au kukosa utulivu basi na si vinginevyo kwani Al Masry wanafungika.
 
Back
Top Bottom