Simba SC wana jambo la kujifunza

Bukoba Finest

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2023
Posts
250
Reaction score
315
Timu ya wekundu wa msimbazi wana jambo la kujifunza, haswa nini cha kufanya kipindi cha preseason nini umuhimu wa preseason na Benchi la ufundi linanufaika vipi.

Simba wamepeleka timu uturuki ambapo siku 6 zinatumika katika usafiri 3 kwenda 3 kurudi. Hapo ni wiki moja imepotea safarini ambazo ni siku nyingi sana katika mazoezi.

Wachezaji zaidi ya watano waliachwa Tanzania kwa changamoto mbalimbali wakiwemo maingizo mapya. Je kocha anapaswa kukaa na wachezaji wake haswa wapya kwa muda gani? ni wastani wa wiki 4 ( minimum) mpaka 8 ( maximum).

Kumbe kama preseason wangefanyia Tanzania wangekuwa ndani ya huo muda ili kumpa kocha nafasi ya kutosha kuwafanyia wachezaji assessment.

Itoshe kusema kwamba endapo Simba akapoteza ngao ya Jamii huyu kocha atafukuzwa na sio kwa makosa yake bali ni management mbovu waliyonayo.
 
acha tule bata uturuki hawa wageni.watapewa mfumo maalumu wa mazoezi
 
Ngao ya hisani hata kama wangebaki hapa Bongo kipigo kipo pale pale
 
Hivi uturuki wamefuata Hali ya Hewa, joto au nini zaidi?
 
Wabongo Kila kitu ni Kupinga.

ACHA WAENDE WAKAJIFUNZE WAKAKAE KWENYE MIUNDOMBINU BORA.

Hata wewe unatamani ungekuwa UTURUKI Jiji la Ismail zamani likiitwa Efeso.

Mungu Ibariki Simba
Kati ya Simba na Yanga nani wa kwanza kwenda Turkey??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…