Simba SC yaachana na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha

Simba SC yaachana na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha

Twende taratibu boss. Tumekubaliana pesa ya mwekezaji ni sehemu ya vyanzo vikuu vya mapato.

Sasa twende kwenye swali la pili, mishahara ya wafanyakazi ambayo ndo msingi wa hoja yetu, ni matumizi ya msingi au matumizi ya ziada?
Bahati mbaya sina muda wa kwenda taratibu maana unauliza maswali ambayo majibu yake yako wazi. Kwa nini usitoe hoja yako moja kwa moja ukajibiwa badala ya kuzungukazunguka?
 
Nani kawaambia Simba inaamini tatizo ni kocha? Daah kuwaelewesha vilaza ni kazi mnooo...kocha kaamua kuondoka mwenyewe kashindwaaa kuendelea kufundisha Simba sio kafukuzwa...
 
Bahati mbaya sina muda wa kwenda taratibu maana unauliza maswali ambayo majibu yake yako wazi. Kwa nini usitoe hoja yako moja kwa moja ukajibiwa badala ya kuzungukazunguka?
Tatizo ni unaandika mambo mengi ndo maana nakupunguza ili nikuelewe.
 
Tatizo ni unaandika mambo mengi ndo maana nakupunguza ili nikuelewe.
Naandika mengi ili nicover maswali yako yote ya nyuma na yale yajayo ili tumalizane maana naona unazunguka mno. Napenda kunyooka
 
Naandika mengi ili nicover maswali yako yote ya nyuma na yale yajayo ili tumalizane maana naona unazunguka mno. Napenda kunyooka
Nia inaweza kuwa nzuri ila matokeo yakawa yasiyo na maana. Yaani ukajikuta unaelezea mambo mengi ambayo yanavuruga machache ambayo yangeeleweka kirahisi iwapo yanajibu swali husika.

Nilitaka kukuelewa kwanini ushangae mm kuuliza iwapo Mo yupo tayari kulipa gharama za ziada za mshahara wa Kocha ila mpaka sasa hatujaelewana sababu unanijibu maswali ambayo sijauliza ila unahisi nitauliza.
 
Nia inaweza kuwa nzuri ila matokeo yakawa yasiyo na maana. Yaani ukajikuta unaelezea mambo mengi ambayo yanavuruga machache ambayo yangeeleweka kirahisi. Nilitaka kukuelewa kwanini ushangae mm kuuliza iwapo Mo yupo tayari kulipa gharama za ziada za mshahara wa Kocha ila mpaka sasa hatujaelewana sababu unanijibu maswali ambayo sijauliza ila unahisi nitauliza.
Tutaendelea kuzunguka hapo hapo ila cha msingi mshahara wa kocha siyo "gharama za ziada" maana ni moja ya gharama za msingi za klabu ya mpira. Pesa hiyo inabidi itoke ndani ya bajeti ya klabu na si kutoka kwa mwekezaji au mtu wa pembeni. Kama mshahara wa Benchikha ni milioni 80 unaokuja na kocha msaidizi na kocha wa viungo hiyo si pesa ya kutisha kwa klabu inayotaka kuchukua ubingwa wa Afrika. Tabia ya watu binafsi kulipia mishahara au pesa za uhamisho za wachezaji na makocha ndiyo imekuwa moja ya misingi ya migogoro na mivurugano katika timu maana anayelipa anaendelea kuwa na ushawishi kwa mtu huyo.

Ngoja niishie hapo usije sema naongea mambo mengi.
 
Hapa sasa nimekuelewa, kuwa kuna ilivyo na inavyopaswa kuwa. Ilivyo ni kuwa Mo anasauti kwenye usajili na mishahara ila inavyopaswa kuwa ni namna ulivyoeleza. Nimekuelewa sahihi?
 
Hapa sasa nimekuelewa, kuwa kuna ilivyo na inavyopaswa kuwa. Ilivyo ni kuwa Mo anasauti kwenye usajili na mishahara ila inavyopaswa kuwa ni namna ulivyoeleza. Nimekuelewa sahihi?
Hata hapo juu nilisema "Kama Mo au viongozi wanataja malipo anayotoa Mo mfano ya matangazo ya kwenye jezi kama pesa iliyomlipa Benchikha au usajili wa wachezaji hapo kuna udanganyifu na ulaghai unafanyika"

Hilo la watu binafsi kuleta na kulipia makocha na wachezaji lilikuwa linafanyika siku za nyuma, sina uhakika ni kwa kiasi gani linaendelea hivi sasa. Msingi wa jibu langu kwako ni kuwa kama Mo analipa mishahara nje ya bajeti mbona ripoti za mapato na matumizi haziainishi hayo malipo? Inakuwaje matumizi rasmi na muhimu ya klabu yasiwemo katika ripoti ya mahesabu ya nusu mwaka hata kama malipo yake yalifanywa kwa pesa za wadau?

Jibu la ziada na ndiyo linaendana na kauli yangu hapo juu ni kuwa kama viongozi wamekubaliana na Mo alipie pesa za usajili na/au kocha in exchange kwa matangazo yake kwenye jezi nalo pia ni njia ya kuficha ili isijulikane analipa kiasi gani kwa huduma hiyo huku inaonekana kama fadhila kumbe ni malipo halali ambayo yalitakiwa kufanywa.

Naepuka kutoa ufafanuzi zaidi ili nisiendelee kukuchanganya zaidi. Mwisho wa siku natoa maelezo haya kulingana na ufahamu wangu tu.
 
Tutashangaa jinsi Simba sasa itashinda mechi zote za ligi zilizobaki kwa mzuka mkubwa ila itakuwa too little too late!! Yanga waleeeeee kileleni. Yanga sasa tushinde mechi zote maana mbumbumbu watakuja na moto wa gesi
 
Weka limit ya hisia, hasira za kiwango cha kufikiria kuua usiruhusu, si salama kwa afya ya akili. Unaitwa mchezo wa mpira wa miguu na wewe ni shabiki.
kuna mambo yanakera sana,kiongozi anatenda tofaut na kaul zake,hivi huwa kuna haja gan kila msimu kusajili wacheza 5+ kwa jerojero?utopolo wanatusimanga hovyo huku mtaani hapakalik
 
kuna mambo yanakera sana,kiongozi anatenda tofaut na kaul zake,hivi huwa kuna haja gan kila msimu kusajili wacheza 5+ kwa jerojero?utopolo wanatusimanga hovyo huku mtaani hapakalik
Ni kweli hakukaliki.
 
Back
Top Bottom