Simba SC yaachana na Kocha Mkuu Didier Gomes da Rosa, Thierry Hitimana kuwa kocha kipindi cha mpito

Wakati huu ndg zangu sio wakulaumiana maana yameshatokea chamsingi tukae kupanga timu yetu upya na uzuri zaidi tumeshaelewa tatizo liko wapi.
 
Yanga wamchangamkie kocha huyo
Benchi la ufundi la Yanga limekamilika kila idara! Tuna shida gani sisi mpaka tufikie hatua ya kumchukua kocha wa kukaa jukwaani wakati wa mechi za kimataifa, kutokana na elimu yake ya kuunga unga!!
 
Timu zote duniani zikifanya vibaya anayehusika kutolewa kafara ni kocha,Kocha anaajiriwa ili kuitengeneza timu ipate matokeo mazuri uwanjani, Pryamids walimfukuza kocha aliyepoteza fainali within 24 hour tu ,Giant Al Ahly juzi hapa walitaka kumfukuza Psto........Who is Gomez asifukuzwe yeye ni nani ,Simba ina shida ya kimfumo na makosa ya kimfumo yanaanguka kwa kocha moja kwa moja.
 
100%
 
Ila wakati mwingine kukaa kimya ni busara sana kuliko kujianika,fikiri kabla hujajianika
 
Kocha mkuu huwa anakuja na timu yake, mara nyingi huja na mtaalamu wa viungo, kocha wa makipa, mtaalamu wa saikolojia n.k

Hivyo kocha mkuu akiachia ngazi ni wazi hata jopo lake litaondoka tu...
Pale kila mtu alikuja kivyake.......kumbuka
 
Yeye ni mtunisia na Nabi ni mtunisia huoni ndio alikuwa lango la GSM?

Hukuona wachezaji walikata Moto dakika 45 za mwisho?

Alifeli Sana na ndie alieshauri wachezaji waende kupokea tuzo JKNC
kocha wa viungo ni Mmisri na sio Mtunisia
 
We piga kelele, ila ndiyo kashatimuliwa. Kocha amepewa pre season ya kutosha kuliko makocha wote Bongo, kacheza zaidi ya mechi kumi, kashinda mbili tu! Tena kwa papatu papatu! Mbaya zaidi timu inacheza hovyo kuliko kipindi chochote ndani ya miaka minne! Yaani kuondoka wachezaji wawili tu, ndiyo amepata wenge?! Hana mbinu za maana, alikuwa anatembelea gia ya kishingo! Atupishe tu!
 
Huu si ushuzi mkubwa.......
kama kumbu kumbu zangu zipo sawa huyu jamaa alifungiwa kwa ukosefu wa vyeti
 
Kocha mkuu huwa anakuja na timu yake, mara nyingi huja na mtaalamu wa viungo, kocha wa makipa, mtaalamu wa saikolojia n.k

Hivyo kocha mkuu akiachia ngazi ni wazi hata jopo lake litaondoka tu...
Adel Zrane aliachwa na Pierre Lechantre.

Gomes Da Rosa hakuja na benchi lake la ufundi
 
Nimemsikia Ibrahim masud maestro akidai "huyo kocha wa viungo na magolikipa pia walikosa vigezo (sifa/ elimu) na mechi yao ya mwisho kuruhusiwa kuwepo kwenye benchi ni ile ya Dodoma jiji" .
Adel Zrane ana PhD kwenye sport science anakosaje vigezo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…