Huyu walompa ukocho mkuu binafsi nina mashaka nae ingawa anaweza kuwa na vyeti vya elimu ya kutosha juu ya taaluma yake. Lkn kuwa na cheti na nin unachokifanya kulingana na taaluma yako ni vitu viwili tofauti.
Simuoni kama ni kocha anaweza kuivusha simba na sioni kama ana mbinu zaid za kuisaisia timuz lkn pia sioni kama ni aina ya makocha ambao ana hamasa kwa wachezaji ili kuwahimiza zaidi hasa timu inapokuwa inacheza na ikawa inahitaji matokeo kwa udi na uvumba.
Na hili tuliliona sote wakati wa mechi na wa-Botswana, jamaa alikuwa kasimana tu ni kimya hakuna chochote anachowahimiza wachezaj kufanya hii ilikuwa tofauti na alivyokuwa akifanya kocha wa Wa-Botswana.
Kwa huyu kocha binafsi bado naona pengo.