Simba SC yaitisha mkutano na Waandishi wa Habari hivi punde

Simba SC yaitisha mkutano na Waandishi wa Habari hivi punde

Daah aisee huyo prezda ana maneno machafu huyoo acha kabisa
 
Simba kaporwa point kivipi? Mbumbumbu bhana..! Kwani simba alishinda mpaka apokonywe point ? Acheni ujinga nyie Thimba,.. Mpira unachezwa uwanjani. Mmeshindwa kupambana mnalilia points za club zingine mpewe nyie.. Hivi kulialia hamuoni ni aibu... Mambo hayo ya watoto,.. Akimuona mtu mwingine kabeba andazi anaanza kulilia Kama la kwake japokua hamjui huyo aliyebeba andazi... Sasa nanyi Thimba mmeshindwa kupambana mnaanza kuliharibu [emoji460]
 
Tulikuwa tunasubiri kuchokozwa ili tuwanyooshe vizuri. Si unaona sasa mkwara wetu Simba SC wa kuitisha Mkutano na Waandishi wa Habari umesababisha TFF watuogope na sasa nasikia wamehairisha tena Kikao cha kumjadili Fakhi na kuamua kuwa kwa sasa Simba SC ibaki na hizo points mpaka hapo watakapokutana tena. Mkuu Simba SC ni Chama lingine na kama TFF ya Jamal Malinzi na hao Watendaji wake wangeipokonya tu Simba SC points zake tungekinukisha CAF na FIFA madudu yote ya TFF ambayo bahati nzuri sana Watu wa ndani wa TFF na ambao pia ni Mnyama Mnyamani ( Wapenzi wa Simba wa Kufa Mtu ) wanayajua.

Sasa waambie Chura Churani ( Yanga FC ) wenzio kuwa watulize vipira vyao na waachane kabisa na Simba SC na wajikite sasa katika kuwalipa Mishahara Wachezaji wao na mmoja wapo leo Saa 5 nimemnunulia Chai ya jero maeneo ya Kariakoo na kainywa kwa pupa hadi kaungua Ulimi kwa njaa Kali na sidhani hata kama ataweza kufanya mazoezi.

Njaa zimewatawala tu mnang'ang'ania kushoboke mambo ya Mume wenu Simba SC. Na mwaka huu tuko radhi hata Kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa kufanya lolote ili mradi tu Simba SC tuwe Mabingwa. Tutaroga na tutahonga vibaya sana hadi Ndoo inyanyuliwe kudadadeki zenu Kandambili / Gongowazi nyie.

Mkuu vepeee? Mkwara umesaidia points hazijarudishwa kwa mwenyewe?
 
Baada ya kuonenaka kuwa TFF ya Malinzi, wana Kagera wenzie ( Wahaya ) na Yanga FC wanataka kuiangamiza Klabu ya Simba juu ya points zake na tayari kukiwa na tetesi kuwa huenda leo mchana maamuzi rasmi yakatolewa na Simba SC kupokwa points Uongozi wa Simba umeitisha mkutano wa haraka sana na Waandishi wa Habari katika wanachosema kuwa TFF, wana Kagera ( Wahaya ) na Yanga FC wameamua kumwaga Ugali sasa Simba SC wao wanaenda kumwaga Mboga, Maji ya kunawa, Chumvi, Pilipili ile tuheshimiane hapa mjini kama siyo nchini.

Mpira wa Bongo umeshaharibika leo ndiyo FIFA na CAF watayajua madudu yote ya Malinzi na Watu wake wa TFF.

Hongereni sana Simba SC kwa kuamua Kukinukisha na leo ndiyo leo!
d
 
Mbona mnajadili issues ambayo imeishamliwa tusonge mbele wanasimba tff ya malinzi ni ngumu simba kuwa bingwa hata hizo mechi wakiona tunelekea kupata ubingwa watatukatia rufaa hata kama mechi ilichezwa mwaka jana
 
Baada ya kuonenaka kuwa TFF ya Malinzi, wana Kagera wenzie ( Wahaya ) na Yanga FC wanataka kuiangamiza Klabu ya Simba juu ya points zake na tayari kukiwa na tetesi kuwa huenda leo mchana maamuzi rasmi yakatolewa na Simba SC kupokwa points Uongozi wa Simba umeitisha mkutano wa haraka sana na Waandishi wa Habari katika wanachosema kuwa TFF, wana Kagera ( Wahaya ) na Yanga FC wameamua kumwaga Ugali sasa Simba SC wao wanaenda kumwaga Mboga, Maji ya kunawa, Chumvi, Pilipili ile tuheshimiane hapa mjini kama siyo nchini.

Mpira wa Bongo umeshaharibika leo ndiyo FIFA na CAF watayajua madudu yote ya Malinzi na Watu wake wa TFF.

Hongereni sana Simba SC kwa kuamua Kukinukisha na leo ndiyo leo!
Ulishaliwa kiboga wewe huko Kaitaba, tulia.
 
Back
Top Bottom